Licha ya kusemwa sana kwa muda mrefu juu ya kuhusishwa na chama kipya cha siasa cha ACT-Tanzania dhidi ya aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Ruyagwa Kabwe (pichani juu akisaini kitabu baada ya kupewa kadi) sasa yamekuwa kweli kwa Mbunge huyo baada ya jana Jumamosi ya Machi 21, kupokelewa rasmi na chama hicho na kukabidhiwa kadi yake yenye namba 007194.
Hili limetokea siku moja tu baada ya Zitto kutangaza kuachia ubunge na kuandika barua rasmi ambapo sasa amekuwa mwanachama wa ACT-Tanzania na kuahidi kuendeleza mapambano ndani ya chama hicho.
ACT-Tanzania: kirefu chake ni Chama cha Alliance for Change and Transparence Makao makuu ya chama hicho yapo Kijitonyama Jijini Dar es Salaam, Tanzania.
nahitaji card haraka sana nitaipataje ikiwa niko ughaibuni???
ReplyDeleteHapo Zitto kadhihirisha kuwa wapinzani kamwe hawashinda kura ya urais tanzania 2015 na daima. Maana wananchi wa kigoma aliwawakilisha kama mbunge watahama chadema na kuhamia ACT- Tanzania. ACT siyo chama chenye nguvu kwa sasa Tanzania, ni zitto tu anataka ubunge tena 2015. Sasa Watanzania lazima mkubali uroho wa madaraka sio CCM tu hata wapinzani.
ReplyDeleteZitto alifukuzwa uanachama Chadema.
ReplyDeleteZitto hakufukuzwa. Katiba ya chadema inasema "mwanachama akiipeleka chadema mahakamani akashindwa, atakuwa amejivua uanachama wake" kwa hiyo alivyoshindwa mahakamani automatically anakuwa sio mwanachama tena.
ReplyDelete