Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

IDARA ya Uhamiaji nchini,Imesema inaendelea kupambana na uhamiaji haramu nchini na kuwataka wananchi waendelee kutoa taarifa za wahamiaji haramu na hatua zinachukuliwa dhidi ya wahamiaji hao.

Hayo ameyasema,Naibu Kamishina wa Idara ya Uhamiaji na Msemaji wa Mkuu wa Idara hiyo,Abbas Irovya ,amesema idara ya uhamiaji inaendelea kupambana na wahamiaji haramu na kufanya uhamiaji haramu kupungua.

Irovya amesema kuwa kuna gazeti moja la wiki jina tunalihifadhi liliandika habari yenye kichwa cha habari kisemacho uhamiaji wanauza nchi kutoka kwa mtoa taarifa Ajazi Ahmed Raia wa Pakistani,idara hiyo inasema mtu huyo aliondolewa nchini tangu mwaka jana.

Amesema Ajazi Ahmed alikuwa kazi yake nchini ni kuingiza wahamiaji haramu ambapo alihukumiwa na mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kifungo cha miaka 18 au faini ya Sh.milioni tano ambapo mtuhumiwa alilipa kwa taratibu za kimahakama na kuondolewa nchini kwa kushirikiana na ubalozi wa Pakistan nchini.

Amesema kutokana na taarifa hizo wananchi wametakiwa kuupuza habari hizo kutokana na kukosa msingi dhidi ya  mtu huyo ambapo aliondolewa nchini kutokana na usafirishaji wa wahamiaji haramu.

Irovya amesema wahamiaji haramu wamekuwa wakitoka nchi 47 zikiwemo nchi za Afrika huku Ethiopia ikiongoza kwa kuwa na wahamiaji wengi kuliko nchi nyingine na wengine wana kesi wako katika magereza yetu nchini.

“Tuko hapa kwa kutoa huduma taarifa hizo hazina ukweli na kama kuna mtu katumika kutoka idara yetu hatua zitachukuliwa dhidi yake kutokana na utaoaji taarifa za uongo kwa jamii kutoka katika chombo cha serikali,amesema Naibu Kamishina Irovya.
Naibu Kamishina wa Idara ya Uhamiaji na Msemaji wa Mkuu wa Idara hiyo,Abbas Irovya (kulia) akizungumza na waandishi wa habari,kwenye ofisi za Uhamiaji,jijini Dar es salaam leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...