Na Bakari Issa,Dar es Salaam
Naibu Kamanda wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM),Wilaya ya Moshi vijijini,Innocent Melleck amempongeza Rais Jakaya Kikwete na Serikali kwa ujumla kwa kuwajali wananchi wa kijiji cha Mwakata wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga waliopatwa na janga la kubomokewa na nyumba zao kutokana na mvua iliyoambatana na mawe makubwa na upepo mkali.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam,Melleck amesema kitendo cha Rais Kikwete kuahidi kuwajengea nyumba wananchi hao kinaonyesha namna anavyowajali wananchi hao.
Melleck ambaye amejitolea kuingia katika kinyanganyiro cha kuwania ubunge jimbo la Vunjo mkoani Kilimanjaro kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM),amesema Serikali ya Rais Kikwete imewasaidia wananchi waliopatwa na majanga mbalimbali wakiwamo wananchi wa Mbagala na Gongo la Mboto waliolipukiwa na mabomu.
Aidha,Melleck amewapongeza viongozi wa CCM kwa juhudi kubwa zinazofanywa na Katibu Mkuu wa CCM,Abrahamani Kinana na Katibu Mwenezi na Itikadi,Nape Nnauye ambao wamefanya kazi kubwa ya kuimarisha Chama huko mikoani na kuweza kuwa viongozi wa kwanza kuzunguka na kuwafikia wananchi.
Pia,Melleck amesema viongozi wamekuwa kiungo kikubwa sana kwa vijana na kutoa mwanga mpya wa nafasi za vijana katika nafasi za uongozi kuwa kubwa pasipo kuwa na upendeleo wowote,na kusema kuwa juhudi na ushirikiano wao ndiyo unaoleta taa ya kijani kwa vijana kuanzia ngazi za chini hadi ubunge.

Naibu Kamanda wa UVCCM Wilaya ya Moshi vijijini, Innocent Melleck akizungumza na waandishi wa habari.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...