Na  Bashir   Yakub.
Watu  wengi  wanaonunua  ardhi  wamekuwa  wakipata  usumbufu  mkubwa katika   kubadili  majina  yaani kutoka  mmiliki  wa  mwanzo  kwenda  kwa  mmilki mpya  aliyenunua. Upo  usumbufu ambao  husababishwa   kwa  makusudi na  maafisa  wanaohusika   lakini  pia  upo  usumbufu  ambao  husababishwa   na  watu  wenyewe  wanaotaka  kubadili  majina.  Awali  ya  yote  lazima  nikiri   kuwa  baadhi  ya  maafisa  wa  mamlaka  za  ardhi  husababisha  uchelewaji  kwa  makusudi  kabisa  na lengo  likiwa kujenga  mazingira   ya  kupozwa kidogo. 
Hili  lipo  na  kila  mtu  ambaye  amekuwa  akishughulikia  masuala  ya  hati  na  kubadili  majina  miliki   kama  mimi  atakiri  kukutana  na  haya.  Hao  tuwaache  mimi  leo  nazungumzia  maandalizi  ambayo  ukiyafanya  mapema  utafanikiwa  kwa  urahisi na  haraka  kubadili   jina  la  kiwanja  au  nyumba  kutoka  kwa  mtu akiyekuuzia  kuingia jina  lako.


1.UMUHIMU  WA  KUBADILI  JINA  HARAKA  BAADA  YA  MANUNUZI.
Sheria  iko  wazi kuwa  ambaye  jina  lake  linaonekana  kwenye  hati  ndiye  mmiliki.

Kwa  kauli  hii   mnunuzi  anatakiwa  kufanya  jitihada  za  haraka  na za  makusudi  kubadili  jina  mara tu baada  ya  kununua  kiwanja  au  nyumba. Sikatai  kuwa  kunakuwa  na  mkataba wa  mauziano  lakini  lazima  ieleweke  kuwa  mbele  ya  macho  ya  sheria   jina  lililo  kwenye  hati  lina  uzito  kuliko  mkataba  wa  mauziano. 
Usiridhike  kukaa  na  mkataba  wa  mauziano  ikiwa  hujabadili  jina. Hii  ni  kwa  ajili  ya  ulinzi  wako  na  wa  ardhi  yako.  Utakapotokea  mgogoro   wa  umiliki  ikiwa  hujabadili  jina waweza  kuwa  katika  hatari  kubwa  ya  kupoteza  hasa  kama  mgogoro  huo  umeanzishwa  na  aliyekuuzia. Huu  ndio  ukweli  na  lazima  tuonyane  ili    tuwe  salama na  mali  zetu. 
Lakini pia  hata  ukitokea  mgogoro  mwingine  wowote  wa  umiliki  kuna  mambo  ndani  ya  sheria  yataufanya  kuwa   mgumu kutokana  na sababu  tu  kuwa ulikuwa  hujabadili   jina.  
Hapo  sijaongelea  faida  nyingine  za kubadili  jina  kama  kukopa  n.k. Nishauri  tu  kwa  ufupi  kuwa  unapojiandaa  kununua  nyumba  au kiwanja  jiandae  pia na  kubadili  jina  moja  kwa  moja.  Hakikisha  haya  mawili  yanakwenda   pamoja. Kusoma zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...