Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokea kadi na bendera za
aliyekuwa Katibu Mwenezi wa Chadema Wilaya ya Longido ambaye amejiunga
na CCM kwenye mkutano uliofanyika Eworendeke.Ndugu Kinana akiwa
ameongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wako kwenye
ziara ya siku tisa mkoani Arusha ya Kuhimiza,kuimarisha na kutekeleza
Ilani ya uchaguzi ya ccm ya mwaka 2010 ikiwemo pia na kusikiliza
matatizo ya Wananchi na kuyapatia ufumbuzi.
Wananchi
wa kijiji cha Eworendeke wakiwa wamekusanyika wakimsikiliza Katibu Mkuu
wa CCM,Ndugu Kinana alipokuwa akiwahutubia wilayani humo.
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Eworendeke
ambapo alitoa salaam za shukrani kwa CCM wilaya ya Longido kwa kuipa
ushindi mzuri wakati wa uchaguzi.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa ujenzi wa nyumba ya watumishi wa Afya katika kijiji cha Lesingeita,wilayani Longido.Pichani shoto ni Mbunge wa jimbo la Longido Mh.Lekule Laizer.
Mzee
Kitasho Simel Nakutamba akimpa mkono Katibu Mkuu wa CCM ndugu
Abdulrahman Kinana mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika hoteli
yake ya Longido kama ionekanavyo pichani.
Pichani ni jengo la kituo cha mafunzo cha Learning In Longido (LIL),ambapo Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana aliweka jiwe la msingi na kushiriki kupaka rangi kwenye
majengo hayo.
PICHA NA MICHUZI JR-LONGIDO ARUSHA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...