Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Profesa John Nkoma (kulia) akimkabidhi rasmi leseni ya kurusha matangazo ya redio ya JEMBE FM ya jijini Mwanza, Mkurugenzi Mkuu wa Jembe FM, Dk Sebastian Ndege (katikati) katika hafla fupi iliyofanyika makao makuu ya ofisi za TCRA jijini Dar. Kushoto ni Mkurugenzi wa sheria wa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA), Fortunata Mdachi.
Mkurugenzi Mkuu wa Jembe FM, Dk Sebastian Ndege akitoa neno la shukrani ambapo pia maeahidi kuwa atafuata masharti na kanuni zote zilizowekwa na mamlaka hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Profesa John Nkoma (wa pili kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na uongozi wa juu kabisa wa Jembe Media Limited. Kutoka kushoto ni Mwanasheria wa Jembe Media Ltd. Justine Ndege, Mkurugenzi Mkuu wa Jembe FM, Dk Sebastian Ndege pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Jembe Media Ltd, Renata Ndege.
Mkurugenzi Mkuu wa Jembe FM, Dk Sebastian Ndege na Mwanasheria wa Jembe Media Ltd. Justine Ndege wakionyesha leseni hiyo iliyoambatanishwa na miongozi ya Mamlaka ya Mawasiliano ya TCRA.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...