Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikatisha kwenye migomba alipokuwa akikagua mifereji ya inayotiririsha maji kuelekea kwenye mashamba ya ndizi akiongozana na Mh. Agrey Mwanri.

Akielezea utekelezaji wa ilani ya uchaguzi katika jimbo hilo Mh. Agrey Mwanri amesema ilani ya CCM imetekelezwa kwa kiwango kikubwa ambapo vijiji vyote katika jimbo hilo vina maji safi na salama ya kunywa, Umeme umefika katika vijiji vyote kinachondelelea ni usambazaji kwa kila mwananchi, Suala la huduma za afya nalo liko vizuri kwani vimejenga vituo vya afya karibu kila maeneo na baadhi ya zahanati zinamaliziwa kujengwa.
Suala la Elimu wakati mbunge huyo akiinga madarakani Siha kulikuwa na sekondari moja, lakini sasa kuna sekondari 17 na ufaulu wa wanafunzi umeongezeka kwa kiwangi cha juu, Maabara zinakamilishwa ambapo mabati yamesambazwa karibu kila shule ili kukamilisha ujenzi wa maabara hizo.
Akizungumza katika mkutano huo pamoja na mambo mengine Katibu Mkuu wa CCM amemsifu Mh. Agrey Mwanri kwa kazi aliyoifanya katika jimbo hilo kwa kufanya kazi vizuri na kuwaletea wananchi maendeleo na kuwaambia wananchi katika mkutano huo kwamba kama kiongozi anafanya kazi nzuri hakuna haja ya kubadilisha viongozi kama mashati, Mwacheni awaleteeni maendeleo.Katika ziara hiyo Kinana anaongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akitoka kwenye chumba cha maabara cha hospitali ya wilaya Siha mara baada ya kuyakagua magari matatu ya kubebea wagonjwa.
Sehemu ya jengo la hospitali hiyo ya wilaya ya Siha kama lionekanavyo pichani,ambapo Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alikwenda kukagua.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...