Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara
jioni ya leo katika uwanja wa sabasaba, wilayani Kondoa, wakati wa ziara
ya siku tisa iliyomalizika leo mkoani Dodoma ya kuimarisha uhai wa
chama, kukagua miradi inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya
CCM, pamoja na kusikiliza kero za Wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
Katika
ziara yake hiyo aliyoambatana na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape
Nnauye ilikuwa ya mafanikio makubwa, kwani msafara wake umetembelelea
Wilaya 7 na majimbo 9 ya uchaguzi kwa kuzunguka jumla ya Km, 2289.
Akizungumza
katika mkutano wa kuhitimisha ziara hiyo mjini Kondoa, Nape alisema
kuwa katika mkoa huo tayari wamefanya mikutano 91, ambapo 82 ya hadhara
na 9 ya ndani. Pia wamekagua jumla ya miradi 73 ikiwemo 62 ya maendeleo
na 11 ya chama,Nape akaongeza kuwa katika ziara hiyo imefanikiwa
kuongeza wanachama wapya wapatao 8245
Kesho
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na Nape Nnauye wanaanza ziara ya kikazi
katika Mkoa wa Arusha, ambapo wataanzia Jimbo la Monduli linaloongozwa
na Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa ambaye ni mbunge wa jimbo hilo.
Mbunge
wa Jimbo la Kondoa, Zabein Mhita akijiandaa kupiga magoti ikiwa ni
ishara ya kumuomba Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana kusaidia kutatua
tatizo la maji katika Mji wa Kondoa
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi,Nape Nauye akihutubia katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa sabasaba,jioni ya leo wilayani Kondoa.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara katika
Kijiji cha Kinyasi, Kata ya Kwadelo, ambapo amemshauri Waziri wa
Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu na Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi pamoja na wakuu wa mikoa minne ya
Dodoma, Manyara, Morogoro na Tanga kukaa pamoja kupata suluhisho la
migogoro inayoendelea ya Wakulima na Wafugaji pamoja na askari wa
Wanyamapori kuwashambulia wananchi na hata kufikia kuwaua kwa risasi
ambazo maganda yake walimuonesha Komredi Kinana katika mkutano huo.
Baadhi ya Wananchi wa Kijiji cha Kinyasi, Kata ya Kwadelo, wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipowahutubia,Kinana amemshauri Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi pamoja na wakuu wa mikoa minne ya Dodoma, Manyara, Morogoro na Tanga kukaa pamoja kupata suluhisho la migogoro inayoendelea ya Wakulima na Wafugaji pamoja na askari wa Wanyamapori kuwashambulia wananchi na hata kufikia kuwaua kwa risasi ambazo maganda yake walimuonesha Komredi Kinana katika mkutano huo.
PICHA NA MICHUZI JR-KONDOA
Inatia moyo kuona uhai wa chama unazidi kustawi kutokana na umati wa watu waliojitokeza. Natumai Mh. Kinana na ujumbe wake, mkiwa njiani kuelekea Arusha, angalau na hapo KOLO WASI msiwasahau kabla hamjapanda kilima cha Dinu.
ReplyDeleteKama nchi inaongozwa na viongozi wanaotaka kupigiwa magoti ili wananchi wapate maji, basi wengi tutakufa kwa kiu!
ReplyDeleteNaona Nape ameanza kutumia alama ya V. Kuna nini kinaendelea?
ReplyDelete