Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara jioni ya leo katika uwanja wa sabasaba, wilayani Kondoa, wakati wa ziara ya siku tisa iliyomalizika leo mkoani Dodoma ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua miradi inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM, pamoja na kusikiliza kero za Wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.

Katika ziara yake hiyo aliyoambatana na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye ilikuwa ya mafanikio makubwa, kwani msafara wake umetembelelea Wilaya 7 na majimbo 9 ya uchaguzi kwa kuzunguka jumla ya Km, 2289.

Akizungumza katika mkutano wa kuhitimisha ziara hiyo mjini Kondoa, Nape alisema kuwa katika mkoa huo tayari wamefanya mikutano 91, ambapo 82 ya hadhara na 9 ya ndani. Pia wamekagua jumla ya miradi 73 ikiwemo 62 ya maendeleo na 11 ya chama,Nape akaongeza kuwa katika ziara hiyo imefanikiwa kuongeza wanachama wapya wapatao 8245

Kesho Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na Nape Nnauye wanaanza ziara ya kikazi katika Mkoa wa Arusha, ambapo wataanzia Jimbo la Monduli linaloongozwa na Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa ambaye ni mbunge wa jimbo hilo.
 Mbunge wa Jimbo la Kondoa, Zabein Mhita akijiandaa kupiga magoti ikiwa ni ishara ya kumuomba Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana kusaidia kutatua tatizo la maji katika Mji wa Kondoa
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi,Nape Nauye akihutubia katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa sabasaba,jioni ya leo wilayani Kondoa.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Kinyasi, Kata ya Kwadelo, ambapo amemshauri Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi pamoja na wakuu wa mikoa minne ya Dodoma, Manyara, Morogoro na Tanga kukaa pamoja kupata suluhisho la migogoro inayoendelea ya Wakulima na Wafugaji pamoja na askari wa Wanyamapori kuwashambulia wananchi na hata kufikia kuwaua kwa risasi ambazo maganda yake walimuonesha Komredi Kinana katika mkutano huo.
Baadhi ya Wananchi wa Kijiji cha Kinyasi, Kata ya Kwadelo, wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipowahutubia,Kinana amemshauri Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi pamoja na wakuu wa mikoa minne ya Dodoma, Manyara, Morogoro na Tanga kukaa pamoja kupata suluhisho la migogoro inayoendelea ya Wakulima na Wafugaji pamoja na askari wa Wanyamapori kuwashambulia wananchi na hata kufikia kuwaua kwa risasi ambazo maganda yake walimuonesha Komredi Kinana katika mkutano huo.
PICHA NA MICHUZI JR-KONDOA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Inatia moyo kuona uhai wa chama unazidi kustawi kutokana na umati wa watu waliojitokeza. Natumai Mh. Kinana na ujumbe wake, mkiwa njiani kuelekea Arusha, angalau na hapo KOLO WASI msiwasahau kabla hamjapanda kilima cha Dinu.

    ReplyDelete
  2. Kama nchi inaongozwa na viongozi wanaotaka kupigiwa magoti ili wananchi wapate maji, basi wengi tutakufa kwa kiu!

    ReplyDelete
  3. Naona Nape ameanza kutumia alama ya V. Kuna nini kinaendelea?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...