Wananchi
wa Bomang'ombe wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman
Kinana alipowahutubia jioni ya leo katika mkutano wa hadhara uliofanyika
mjini hapo wilayani Hai,mkoa wa Kilimanjaro.
katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akipita kwenye moja ya daraja maarufu sana wilayani Hai,Dara la MNEPO (la zamani) lililopo katika kitongoji cha Kiyungi kijiji cha Mijongweni,wilayani Hai mkoani Kilimanjaro.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akikagua ujenzi wa daraja jipya la MNEPO ambalo lipo katika hatua za mwisho kukamilika,lililopo katika kitongoji cha Kiyungi kijiji cha Mijongweni,wilayani Hai mkoani Kilimanjaro.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza na baadhi ya wakazi jamii ya kimasai kutoka kijiji cha Mtakuja,wilayani
Hai,mara baada ya
kusikiliza mgogoro wao wa ardhi na kampuni ya KADCO,ambapo Ndugu Kinana
ameahidi kuutafutia ufumbuzi mgogoro huo ambao umedumu kwa miaka mingi.
Baadhi ya wakazi jamii ya kimasai kutoka kijiji cha Mtakuja,wilayani Hai,wakimshangilia Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana kwa staili ya aina yake,alipokuwa akiondoka kijijini hapo mara baada ya kuzungumza nao kusikiliza mgogoro wao wa ardhi na kampuni ya KADCO,ambapo Ndugu Kinana ameahidi kuutafutia ufumbuzi mgogoro huo ambao umedumu kwa miaka mingi. SOMA HAPA KUHUSIANA NA MGOGORO HUO
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiongozwa kukagua chumba kipya cha mionzi,pichani nyuma ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Mh.Leonidas Gama.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye akifanya majaribio ya uchunguzi juu ya mkono wake kupitia mashine mpya ya mionzi,iliyowekwa katika chumba hicho cha mionzi.
PICHA NA MICHUZI JR-HAI KILIMANJARO
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...