Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) mkoa wa Lindi,Fortunata Raymond akitoa elimu ya umuhimu na faida ya kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF),kwa viongozi wa chama cha mpira wa miguu na vilabu vilivyopo Manispaa ya Lindi mjini,ambapo aliwataka kutambua na kuchangamkia fursa ya kujiunga na mfuko huo kwani ni wa gharama nafuu,utakaowawezesha kupata huduma za matibabu na familia zao kwa kuchangia mara moja kwa mwaka mzima,elimu hiyo ilifanyika kwenye Uwanja wa Ilulu Mkoani Lindi.
Mwalimu Fikiri ambaye ni mweka hazina wa chama cha mpira wa miguu Manispaa ya Lindi akiuliza jambo kwa mtoa mada ambaye ni Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) mkoa wa Lindi,Fortunata Raymond (hayupo pichani) wakati wa utoaji elimu kwa viongozi hao uliofanyika hivi karibuni kwenye viwanja vya mpira wa miguu ilulu lindi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...