Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

Kampuni ya Kaymu imefungua tawi lake Kariakoo kwa ajili ya wafanyabiashara na wanunuzi kwa njia ya mtandao pamoja na uhifadhi wa bidhaa kabla hazijasafirishwa kwenda maeneo husika, hali ambayo itasaidia kuwapunguzia usumbufu wauzaji waliokubaliana na kampuni hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo,Meneja wa Kaymu Tanzania, Erfaan Mojgani amesema kufungua huduma kwa njia ya mtandao ni kurahisisha uendeshaji biashara pamoja na kuondoa usumbufu kwa mteja wa bidhaa husika.

Amesema kampuni ya Kaymu inaendesha huduma kwa njia mtandao katika nchi 17 za Afrika ambapo wafanyabiashara wanajisajili katika kampuni hiyo kwa ajili ya kufanya biashara kwa njia ya mtandao kwa wateja kuchagua na kufanya manunuzi kwa bei ambayo kila mtanzania anaweza kumudu.

Kwa upande wa Mfanyabiashara wa Viatu katika Maduka ya kariakoo,Zacharia Lucas (Cha Classic) amesema amekuwa na mafanikio katika kupata bidhaa kupitia Kaymu.

“Tumefurahishwa sana na hatua ya Kaymu kufungua kituo chake hapa Kariakoo,kwani italeta mafanikio kwa wafanyabiashara kutokana na kukua kwa teknolojia ya mawasiliano”alisema Lucas.
Meneja wa Kampuni Kaymu nchini,Erfaan Mojgani akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam, juu ya upatikanaji wa bidhaa mbalimbali kwa njia ya Mtandao kwa wanunuzi na wafanyabiashara katika masoko yaliyopo katika mtandao wa kaymu. 
Mfanyabiashara wa Viatu katika Maduka ya Kariakoo,Zacharia Lucas (Cha Classic) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Dar es Salaam (hawapo pichani) juu ya  faida ya kuuza bidhaa zake katika mtandao wa Kaymu.Katikati ni Meneja wa Kampuni Kaymu nchini,Erfaan Mojgani pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Usambazaji wa Kampuni Kaymu,Ulumbi Bryceson. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...