Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (katikati), akishiriki kuchimba shimo
la choo cha Shule Mpya ya Msingi ya Kikwete, eneo la Chamwino Ikulu,
Jimbo la Chilonwa wakati wa ziara yake ya siku tisa ya kuimarisha uhai wa chama,
kukagua miradi inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM,
katika Wilaya ya Chamwino, Mkoa wa Dodoma leo.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akishiriki kupulizia dawa ya kuua wadudu katika mradi wa shamba la zabibu wa Chinangali II, wilayani Chamwino, mkoani Dodoma leo.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye akisalimiana na Mbunge wa jimbo la Mtera,Mh.Livingstone Lusinde ndani ya wilaya ya Chamwino mapema leo.
Sehemu
ya jengo la Zahanati ya kijiji cha Mahampha katika kata ya
Chilonwa,Wilayani Chamwino,ambapo Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana
alishiriki ujenzi wa zahanati hiyo
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiungana na vikundi vya ngoma kupiga
ngoma alipowasili kwenye mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Shule ya
Sekondari ya Majereko, wilayani Chamwino leo.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akihutubia katika mkutano huo wa hadhara.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana Katibu
Mkuu wa CCM,akihutubia katika mkutano huo, ambapo alisema CCM ni chama
pekee nchini kinachowajali wanawake kwa kuwapatia nafasi nyingi za
uongozi. Leo ni maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani ambayo kitaifa imeadhimishwa mkoani Mororo na mgeni rasmi alikuwa Rais Jakaya Kikwete.
PICHA NA MICHUZI JR-CHAMWINO DODOMA.
Copy and WIN : http://bit.ly/copynwin
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...