Tume
ya Taifa ya Uchaguzi inawatangazia wananchi wote wa Mkoa wa Njombe, kuwa
itaanza zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa kutumia
teknolojia ya “Biometric Voters Registration” kuanzia tarehe 16/03/2015 hadi tarehe 12/04/2015. Aidha katika kata ya Utengule ya Mji mdogo wa Makambako Uboreshaji utafanyika kuanzia tarehe 9-15/03/2015. Uandikishaji huo
utahusisha Halmashauri zifuatazo:-
Mkoa
|
Wilaya
|
Kata
|
Idadi
ya Vituo
|
Tarehe
Ya Uandikishaji
|
NJOMBE
|
NJOMBE
TC
|
ZOTE
|
|
16/03 – 12/04/2015
|
|
WANGING’OMBE
DC
|
ZOTE
|
|
|
|
NJOMBE
DC
|
ZOTE
|
|
|
|
LUDEWA
DC
|
ZOTE
|
|
|
|
MAKETE
|
ZOTE
|
|
|
|
MAKAMBAKO
|
UTENGULE
|
12
|
11-17/03/2015
|
Vituo
vya Uandikishaji vitakuwa kwenye Vijiji, Vitongoji na Mitaa
Watakaohusika katika zoezi hili ni wananchi
wote:-
·
Waliotimiza umri wa Miaka 18 na kuendelea na wale wote
watakaotimiza miaka 18 ifikapo mwezi Oktoba, 2015.
·
Waliojiandikisha awali kwenye Daftari la Kudumu la
Wapiga Kura la zamani ili kuhuisha taarifa zao na kupata kadi mpya za kupigia
kura.
·
Wale wote ambao wanazo sifa za kujiandikisha lakini hawajawahi kujiandikisha kwenye
Daftari.
Tume
ya Taifa ya Uchaguzi inasisitiza wananchi wote wa Mkoa wa Njombe kujitokeza kwa wingi kuanzia tarehe 16/03/2015 mpaka tarehe 12/04/2015
kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ili kuwawezesha kupiga
Kura ya Maoni na kuchagua Viongozi wao katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu 2015.
Vituo
vya kujiandikisha vitafunguliwa kuanzia saa 2:00 Asubuhi na kufungwa saa 12:00
jioni
Kumbuka:- Hutaweza kupiga Kura ya Maoni au Kupiga Kura wakati
wa Uchaguzi Mkuu kama utakuwa hujajiandikisha katika Daftari la Kudumu la
Wapiga Kura.
Nenda kajiandikishe sasa.
Tangazo hili limetolewa na
Tume ya Taifa ya
Uchaguzi, S.L.P. 10923, Dar es Salaam
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...