Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Said Meck Sadiki akizindua mradi wa Maji ya Kisima mtaa wa Mongolandege, Ilala jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki ya Maji mkoani Dar es salaam. Mradi wa Kisima hicho umegharimu kiasi cha shilingi milioni 78.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Said Meck Sadiki akifungua moja ya bomba la maji la mradi wa Maji ya Kisima mtaa wa Mongolandege, Ilala jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki ya Maji mkoani Dar es salaam.
Bi. Martha Singano, Mkazi wa Mongolandege akipokea ndoo ya maji kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Said Meck Sadiki mara baada ya kuzindua mradi wa Maji ya Kisima katika mtaa huo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...