Baadhi ya Maafisa, Askari na Mtumishi raia ambaye pia Mhasibu Mkuu wa Jeshi la Magereza Estomih Hamis (Mzee wa Magereza Kileleni) wa saba kutoka kushoto wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuwasili katika kilele cha Mlima Kilimanjaro asubuhi ya Machi 9, 2015 na kutundika bendera ya Jeshi hilo kileleni.
Kiongozi wa Msafara wa Maafisa, Askari na baadhi ya watumishi raia wa Jeshi la Magereza waliopanda mlima Kilimanjaro Kamishna Msaidizi wa Magereza Alexander Mmasy akiwa katika uso wa furaha mara alipowasili katika kituo cha Gilman’s kabla ya kuanza safari ya kuelekea kilele cha Mlima huo cha Uhuru. Kushoto ni Mkaguzi wa Magereza Bakari Boi akiwa katika sura ya uchovu baada ya safari ndefu ya usiku kucha kutoka Kituo cha Kibo kuelekea Gilman’s.
Kundi la Maafisa, askari na watumishi raia wa Jeshi la Magereza pamoja wa waongoza njia (guiders) kwa pamoja likiwa katika mwendo wa kilometa tisa kutoka Horombo kwenda kituo cha Kibo ambapo liliwasili majira ya saa tisa alasiri na kupumzika kabla ya kuanza safari ya kwenda Gilman’s saa tano usiku.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...