Na Bashir Yakub.
Kuongezeka kwa makampuni na taasisi mbalimbali kumetengeneza wingi wa
ajira maeneo mbambali ya nchi. Mbali na kuongezeka kwa ajira hizi
kumekuwepo na tatizo kubwa la waajiriwa kutojua haki zao mbalimbali
wawapo maeneo ya kazi.
Niseme jambo moja tu kuwa hakuna suala la
msingi kama muajiriwa kujua haki zake. Hii ni kwasababu kupitia kujua haki
zake ndipo anapoweza kupata ujira stahiki, posho stahiki, masurufu stahiki,
mafao stahiki, malipo stahiki ya kuachishwa kazi ikiwa ni pamoja na ujumla
wa kufanya kazi kwa misingi ya kazi.
Ni muhimu kila mfanyakazi kupitia pitia haki zake mara kwa mara ili kujua
nini anapata na nini hapati. Uwe kazini au umeachishwa bado ipo nafasi ya
kudai haki hizi ili upate kilicho chako.
Ukitegemea mwajiri ndio akwambie
haki zako utakuwa unajidanganya kwasababu yawezekana kabisa faida
kubwa ya mwajiri ipo katika wewe kutokujua haki zako. Ni hasara kubwa
kufanya kazi bila kujua haki zako . Kutokana na hilo leo nitaeleza baadhi ya
haki za mfanyakazi.
1. HAKI YA KUJUA SEHEMU YA KUFANYIA KAZI.
Isiwe uliambiwa eneo la kazi ni Dar es salaam halafu ujikute kila siku una
safari za mikoani halafu uambiwe eti hiyo ndiyo kazi yenyewe, hapana.
Lazima eneo la kufanyia kazi lijulikane kwa mfanyakazi. Ijulikane kuwa
umeajiriwa na eneo lako la kazi ni Dar es salam , au Mwanza au Kagera.
Hii
ina maana kubwa kwakuwa mfanyakazi asipojua eneo lake la kazi hataweza
kudai malipo yatokanayo na kufanya kazi nje ya ofisi . Lakini iwapo unajua
eneo lako la kazi basi utakapokuwa nje ya eneo la kazi yakupasa kudai
malipo ya ziada. Kwa hiyo hakikisha mwajiri wako unakuainishia kwa uwazi
kabisa eneo lako la kazi na ulijue. Nje ya hilo eneo ni malipo mengine
ambayo ni nje ya mshahara wa kawaida.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...