Na Ahmaid MMOW-Lindi
Kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi oktoba mwaka
huu,Mwandishi wa habari wa kituo cha televisheni cha Channel
ten,Abdulaziz Ahmed leo Ametangaza nia yake ya kugombea ubunge
katika jimbo la Lindi mjini katika uchaguzi mkuu ujao kupitia Chama
cha Mapinduzi (CCM).
Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa,Abdulaziz ambae pia ni
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoani Lindi alisema kuwa
amefikia uamuzi huo baada ya kujitathimini na kugundua kuwa anao uwezo
wa kuzikabili na kuzitafutia majibu yakinifu changamoto mbalimbali
zilizopo katika jimbo la Lindi ambalo kwa sasa lipo chini ya Mbunge
toka CUF,Salum Barwany.
"mwaka 2010 niliomba ridhaa ya kugombea ubunge kupitia Chama Cha
Mapinduzi hata hivyo kura hazikutosha kupitia chama changu na Jimbo
kuchukuliwa na Upinzani na nimeona changamoto nyingi zimeendelea
kuwepo kwa miaka nenda rudi bila kutafutiwa ufumbuzi wa uhakika Nipeni
Ridhaa wana lindi niwatumikie kuliko ilivyotokea katika matarajio yenu
2010-2015".
Aidha alibainisha changamoto hizo ni pamoja na miundombinu ya
barabara,maji,huduma za afya na umeme usio na uhakika huku Akiainisha
kuwa nguvu na uwezo wake kushinda katika kura za maoni ndani ya Chama
Cha Mapinduzi na uchaguzi mkuu zipo mikononi mwa wananchi wa jimbo
hilo na ambao wanakiu
ya maendeleo na mabadiliko.
" sitegemei kutumia Fedha ili kuwa nunua wapiga kura bali wale wapenda
maendeleo na mabadiliko ndiyo mtaji na silaha yangu,rushwa hapana
kwani chama chetu hakitaki kabisa kitendo hicho kwa kuwa kinaathiri
Maendeleo na kinaua chama cha Mapinduzi kwa Uwepo wa Makundi
yanayotaka kupona maisha yao tu si maendeleo.
Aidha alitoa wito kwa Vijana kujitokeza kwa wingi kujiandikisha huku
wengine wakijiunga na Chama hicho ili kumpigia kura Mgombea ambae
anatoka katika kundi la Vijana kwa kuwa Vijana ndio Taifa la leo.
Sambamba na hilo Abdulaziz aliziasa kamati za chama na vikao vya
uteuzi kuzingatia matakwa na maamuzi ya wanachama huku akikemea matumizi
ya fedha kwa wagombea kuhonga wanachama ili wawapigie Kura.
"Mpango huu wa kuhonga wanachama una athari kubwa kwa Chama Pia upo
uwezekano wa kupata mgombea asiekubalika na kuendelea kutwaliwa na
Upinzani ni lazima tuwe makini katika hili,Nina Imani hata Vijana toka
vyama vya Upinzani wataniunga mkono na kunichagua
kuwawakilisha".Alimalizia Abdulaziz alipokutana na waandishi wa habari
wa Vyombo Mbali mbali
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...