Na Victor Mariki – Ofisi ya Makamu wa Rais.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Dk. Binilith Mahenge ameishauri
Halmashauri ya Jiji la Mbeya kutafuta wawekezaji watakaotumia taka kama malighafi
katika shughuli uzalishaji viwandani ili kukabiliana na uchafuzi wa mazingira jijini
humo.
Ushauri huo aliutoa, akiwa katika ziara ya siku mbili mkoani humo wakati
alipotembelea Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mbeya na kuzungumza na Idara ya
Usafishaji na Mazingira jiji humo jana.
Aliongeza kusema kuwa taka ni mali, zinaweza kutumika katika uzalishaji wa
bidhaa nyingine huku akitolea mfano Kiwanda cha Falcon, kinachozalisha milango
pamoja na chemba za vyoo kwa kutumia taka huko jijini Mwanza.
Pia katika ziara hiyo Mh. Mahenge, alitembelea Mtaa wa Ntungi, Kata ya
Nsalaga ili kuona ujenzi wa dampo jipya lenye mita za ujazo 454,000, linaloweza
kutumika ndani ya miaka sita ambalo ujenzi wake umewezeshwa na Benki ya Dunia kwa
gharama ya shilingi bilioni 3.8.
Wakati huo huo pia, alitembelea hifadhi ya Safu ya Mlima Mbeya ili kujionea
mikakati ya utunzaji mazingira inayotekelezwa katika hifadhi hiyo, ikiwemo upandaji
miti kwa ajili ya kutunza vyanzo vya maji pamoja na ugawaji wa mbegu ya miti ya kuni
bure kwa wananchi waishio karibu na hifadhi ili kuhepusha vitendo vya ukataji miti
katika hifadhi hiyo.
Katika majumuisho ya ziara yake mkoani Mbeya, Mh. Mahenge alitembelea
kiwanda cha saruji cha Mbeya Ciment, ambapo aliridhishwa na uendeshwaji wa shughuli
za uzalishaji kiwandani hapo nakuupongeza uongozi wa kiwanda hicho kwa kuzingatia
Kanuni za Mazingira.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Injinia Binilith Mahenge (katikati), akitoa majumuisho wakati akimalizia Ziara yake ya Siku mbili iliyofanyika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Mbeya nakumalizikia katika Kiwanda cha Saruji kilichopo eneo la Songwe, Mkoani humo jana. (Picha na OMR)
Saruji ipungue bei Mbeya, kiwanda kipo kwetu saruji wanatuuzia bei sana tofauti na mikoa mingine. Mfuko mmoja 16,000 wakati Dar 14, 000 sijui kipi tofauti wanatungonga sana Mbeya jamani.
ReplyDelete