Na Chalila Kibuda ,Globu ya jamii

Jeshi la polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, linaendelea na uchunguzi dhidi ya Mlinzi wa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Dk.Wilbrod Slaa anayedaiwa kufanya njama ya kumuua kwa sumu, Bw. Khalid Kagezi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo,Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova amesema wamechukua maelezo kwa Katibu Mkuu Dk.Wilbrod Slaa pamoja na maelezo ya mlizi wake Khalid Kagezi.
Kamishina Kova amesema Chadema walichukua hatua mbalimbali na kujiridhisha kuhusika kwa mlinzi wa Dk.Slaa kufanya mikakati ya kumuua kwa sumu kwa kuiweka katika maji au chakula.
Amesema kwa maelezo ya Mlinzi huyo alidai kuteswa na baadhi ya watu wa chama cha Demokrasia na Maendeleo kwa kuwataja kwa majina.
 Kamishina Kova amesema Kagezi alidai kutekwa na kushambuliwa katika mwili wake na jeshi la Polisi likampa fomu namba tatu (PF3)kwa ajili ya matibabu
“Jeshi la Polisi limefanya jitihada kwa kupata maelezo kwa watu wote ambao wamehusika kwa mlizi na Dk.Slaa”amesema Kamishina Kova.
Amesema baada ya uchunguzi watapeleka kwa wakili wa serikali na yeyote atakayehusika sheria itashika mkondo wake.
Wakati huo huo, Haroub Mtopa anashikiliwa na jeshi la polisi kwa kufanya utapeli katika ofisi ya Rais kwa kudai kuwa yeye ndiye Katibu wa Rais  Bw. Prosper Mbena.
Mtopa amekamatwa jana baada ya kutegeshewa mtego wa sh.250,000 za jeshi la polisi kwa mtu anayedaiwa kutapeliwa kutaka kumuongeza fedha kwa mara ya pili.
Kamishina Kova amesema Mtopa alikuwa kila siku anapita Ikulu kwa matatizo mbalimbali kumbe ndio alikuwa akiwatega watu na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.
Amesema watu wanaofika katika ofisi zote bila kuwa na taarifa zao wawafatilie kutokana na kufanyia utapeli kupitia ofisi hizo
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Kamishna Suleiman Kova akizungumza na Waandishi wa Habari ofisini kwake leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...