Na Happy Shirima - Habari Maelezo.

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo [WAMA] anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani yatakayofanyika Machi 8 mwaka huu katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam .

Akizungumzia maadhimisho hayo leo jijini Dar es salaam , Kaimu Mkuu wa mkoa wa Dar se salaam Mhe. Raymond Mushi amesema kuwa maadhimisho hayo mwaka huu yataongozwa na kauli mbiu isemayo “Uwezeshaji Wanawake Tekeleza, Wakati ni Sasa “.

Amesema ujumbe huo unaikumbusha jamii kujenga mazingira  wezeshi kwa kutambua mchango wa wanawake katika kuleta maendeleo ya jamii na nchi kwa ujumla .

Ameeleza  kuwa wadau kote nchini wanatakiwa kuelimishwa ili kuangali upya wajibu wao kwa kuwashirikisha, kuwaamini na kuwapa wanawake haki sawa katika nafasi za elimu , uchumi na uongozi ili waweze kuwa chachu ya maendeleo yao binafsi, familia na taifa zima.

“Lengo la maadhimisho haya ni kukumbuka wajibu wa kila mmoja  kushiriki katika mikakati  ya kukabiliana na changamoto mbalimbali za wanawake kuanzia ngazi ya kaya hadi Taifa” Amesema.

Akitoa ufafanuzi kuhusu maadhimisho hayo amesema kuwa yanaambatana na maonyesho ya kazi na bidhaa mbalimbali za vikundi vya ujasiriamali na kuzishirikisha Asasi za Kiraia  zinazojishughulisha na masuala ya utoaji wa Elimu ya Uraia na sheria ya utunzaji fedha.

Ameongeza kuwa siku ya kilele  kutakuwa na maandamano yatakayoanzia Barabara ya Lumumba na kuishiaviwanja vya mnazi mmoja ambayo yatapokewa na mgeni rasmi  na wananchi  wa mkoa wa Dare s salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Our first lady looks beautiful.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...