Uongozi wa TTCL ukitoa Msaada wa Madawati katika Shule ya Msingi Bunena leo Ijumaa.TTCL inaamini kutoa msaada huo wa Madawati utasaidia kuboresha Ufanisi wa Shule na hatimaye kupata Matokeo Makubwa sasa katika Sekta ya Elimu. Pia ni Mategemeo ya TTCL kuwa utaleta chachu kwa wadau wengine katika Sekta kuweza kuchangia katika sekta hiyo pana ya Elimu. Hatimae kuondoa Changamoto zinazoikabili sekta ya Elimu hapa Mkoani Kagera na Nchi nzima kiujumla. TTCL pia imeweza kuwahakikishia wadau mbalimbali waliohudhuria hafra hiyo kuwa wataendelea kuwa bega kwa bega katika kuleta maendeleo kadri hali ya kifedha itakavyoruhusu.

Wanafunzi wakikalia dawati moja wapo ambapo dawati moja litakaliwa na Wanafunzi 3 hivyo madawati hayo yatawatosha wanafunzi 150 wa Shule hiyo ya Bunena.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...