Mkurugenzi Mtendaji wa Muda wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Pius Tibazarwa (katikati) akikabidhi funguo kwa mshindi wa zawadi kubwa ya promosheni ya Weka Upewe, Josephat Ruyongo mkazi wa Bukoba, ya gari lake jipya alilojishindia la Nissan Hardbody katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa NBC, Mussa Jallow. Gari hilo lina thamani ya zaidi ya sh milioni 54.
Mshindi wa zawadi kubwa ya promosheni ya Weka Upewe ya Benki ya NBC, mkazi wa Bukoba, Josephat Ruyongo akifungua gari lake mara baada ya kukabidhiwa rasmi na Mkurugenzi Mtendaji wa Muda wa NBC, Pius Tibazarwa (katikati), jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa NBC, Mussa Jallow.
Mshindi wa zawadi kubwa ya promosheni ya Weka Upewe ya Benki ya NBC, mkazi wa Bukoba, Josephat Ruyongo akiwasha gari lake tayari kwa safari ya Bukoba mara baada ya kukabidhiwa jijini humo leo.
Mshindi wa zawadi kubwa ya promosheni ya Weka Upewe ya Benki ya NBC, mkazi wa Bukoba, Josephat Ruyongo (katikati) akipozi kwa picha ya kumbukumbu pamoja na baadhi ya maofisa wa benki hiyo mara baada ya kukabidhiwa gari lake.
Hongera mshindi kwa kukabidhiwa zawadi ya gari. Promosheni hizi ni nzuri.
ReplyDeletejamani itabidi afundishwe kuendesha kabla hajapewa gari. maana ajali kibao siku hizi.
ReplyDeleteni hayo tuuuu.
asante
Msemakweli