Na Anitha Jonas-MAELEZO,Dodoma.

Waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya amesoma Muswada wa Sheria ya Mifumo ya Malipo nchini wa mwaka 2015 kwa mara ya pili Bungeni Mjini Dodoma,Sheria hii imelenga kudhibiti wizi unaofanyika kupitia mitandao pamoja na kuhakikisha serikali inanufaika kwa kujipatia mapato.

Mhe.Mkuya alisema chimbuko la Muswada huo ni matokeo ya maboresho yaliyofanywa na Serikali katika sekta ya fedha nchini yaliyoanza mwaka 1990 na yanayoendelea mpaka sasa pamoja na maboresho katika sekta ya fedha yaliyosababisha kutungwa kwa sheria ya mabenki na taasisi za fedha za mwaka 2006 pamoja na sheria ya Benki kuu ya mwaka 2006.

“Lengo la Muswada huu ni kuboresha Usimamizi,Udhibiti na Kuimarisha Mifumo ya Malipo nchini,pamoja na kuiweka nchi katika mazingira mazuri ya ushindani wa kibiashara,halikadhalika kudhibiti changamoto zinazoweza kutokea katika sekta ya fedha na kutengeneza mazingira bora ya kiufanisi,”alisema Mhe.Mkuya.

Kwa upande wa maoni ya Kamati ya Upinzani yaliyosomwa na Mhe.Christina Lissu (Viti Maluum -CHADEMA) kwa niaba ya Mwenyekiti wa kambi ya upinzani ya Wizara ya Fedha Mhe.James Mbatia,Kamati ilishauri Serikali kuondoa ukomo wa faini na badala yake iwe inasomeka (zaidi ya) kwa ajili ya kumwachia Hakimu kupanga ukomo wa faini hiyo,hivyo serikali ifanye mabadiliko katika cha 20 (a) na (b).

Katika kipindi cha uchangiaji wa maoni Mhe.Musa Azza (Mb) wa Ilala naye aliishauri serikali kuunda chombo kitakacho simamia mihamala yote inayofanywa kupitia mtandao ili serikali iweze kujipatia mapato ambayo yatasaidia kuendeleza nchi yetu tofauti na sasa fedha nyingi zinapotea na serikali inakosa mapato.

Naye Mhe.Suzan Lyimo Mbuge wa Viti Maalum Chadema aliishauri serikali kuwa sheria hii iangalie suala la mifumo ya mtandao kuwa chini kwani hili limekuwa liliwagarimu sana wananchi,halikadhalika gharama zinazotozwa na makampuni ya simu katika Kutoa Pesa na Kuhamisha Pesa kama Mpesa,Tigopesa na Airtel Money.

Muswada huu na jumla ya sehemu 12 na Ibara 59 ambazo zimezingatia kuleta manufaa makubwa kwa wananchi pamoja kuiletea mapato serikali.
Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera na Uratibu na Bunge Mhe.Jenista Mhagama (Mb) akimsikiliza kwa makini Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.William Lukuvi wakati wa kikao cha bunge kikiendelea Mjini Dodoma.
Waziri wa Fedha Mhe.Saada Mkuya akisoma Muswada wa Sheria Mifumo ya Malipo wa Mwaka 2015 katika Mkutano wa 19, Kikao cha Sita Mjini Dodoma.
Naibu Waziri wa Maji Mhe.Amos Makalla akijibu swali kwa lililoulizwa na Mhe.Prof.David Mwakyusa (Mb) wa (Rungwe Magharibi) Bungeni Mjini Dodoma.
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mhe.Anne Kilango akijibu swali liliulizwa na Mhe.Amina Makilagi Mbunge wa Viti Maalum lilohoji juu ya mchang’anuo wa ada za Vyuo vikuu vya Umma,Bungeni Mjini Dodoma .Picha zote na Anitha Jonas-MAELEZO,Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...