Na Mwandishi Wetu, Dodoma
MBUNGE wa Viti Maalum (CCM), Al Shaimaa Kweigyir, ameitaka
serikali kuhakikisha kwamba hukumu za watu wanaokutwa na hatia dhidi ya watu
wenye ulemavu wa ngozi (albino), zinafanyika kwa uwazi, sambamba na
kutocheleweshwa ili kulinda roho za Watanzania wanaoendelea kuangamia.
Al-Shaimaa aliyasema hayo bungeni jana wakati akitoa maelezo binafsi
kwa kupitia Kanuni ya Kudumu ya Bunge ya (50) 1 inayomtaka mbunge kwa ruhusa ya
Spika kutoa maelezo binafsi yanayomhusu au yanayoigusa jamii moja kwa moja.
Mbunge huyo ambaye pia ni mlemavu wa ngozi alisema kwamba
endapo hukumu za kesi za wahalifu wa albino zitahukumiwa mapema na kwa uwazi
itatoa funzo kwa wengine wanaofikiria kufanya unyama dhidi ya albino hapa
nchini.
Mbunge wa Viti Maalumu, Al-Shaymaa Kweigyir, akiomba mwongozo wa Spika bungeni jana mjini Dodoma, kutaka hatua za haraka zichukuliwe dhidi ya watuhumiwa wa mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino).
Akiendelea kuongea kwa msisitizo juu ya mauaji ya albino Tanzania.
“Na mimi ni mhanga katika jambo hili kwa sababu watu wanaishi
kwa mashaka, hivyo naomba hukumu za wahalifu hao ziwe wazi kila mtu aone ili
iwe fundisho kwa waliofanya na wale wanaofikiria siku moja wajiingize kwenye
unyama huo.
“Pia naomba sheria za mauaji zirekebishwe ili kulinda haki za
walemavu mara baada ya kufanyiwa unyama sambamba na kuwapa adhabu kali wale
wote wanaokutwa na hatia dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi,” alisema
Kweigyir.
Kweigyir ni miongoni
mwa wabunge wanaopigania haki za kuishi za watu wenye ulemavu wa ngozi, likiwa
ni janga lililoshika kasi katika maeneo kadhaa ya Tanzania, hususan katika
mikoa ya Kanda ya Ziwa kunakoonekana kushamiri vitendo vya kuwadhuru na kuwaua
walemavu hao wa ngozi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...