Gari ya Serikali aina ya Toyota Land Cruser yenye namba za Usajili STK 7278, ikiwa imeparamia ukuta wa Shule ya msingi Al Muntazir iliyopo kwenye makutano ya barabara ya Sea View na Barack Obama Drive, jijini Dar es salaam. Kwa mujibu wa mashuhuda dereva wake alijikuta hana jinsi ila kutoka barabarani kuepusha mzinga swa uso kwa uso wakati alipochomekewa ghafla na gari nyingine ya teksi ambayo baada ya kusababisha ajali hii iliingia mitini. Ajali hii imetokea jioni ya leo wakati gari hili likiwa linatokea mjini kuelekea upande wa Palm Beach. Hakuna aliejeruhiwa katika ajali hii.
Wafanyakazi wa "Break Down" wakiangalia namna ya kuichomoa gari hiyo iliyoparamia ukuta wa Shule ya msingi Al Muntazir iliyopo kwenye makutano ya barabara ya Sea View na Barack Obama Drive, jijini Dar es salaam leo.
Hivi ndivyo ionekanavyo gari hiyo mara baada ya kuchomolewa kwenye ukuta huo.
Pole mwenye nyumba
ReplyDelete