Na  Bashir  Yakub.

Nimekuwa  nikiulizwa  maswali  mengi    kila  inapotoka  makala. Nami  nimeweka  ahadi  ya  kukusanya  maswali hayo  na  kuyajibu  na  si  kuyajibu  kwa  kumjibu  mtu aliyeuliza  peke  yake   , hapana  isipokuwa  kwa  kuyaweka  katika   makala  ili  umma  wote  ufaidike.  Haya  ni  baadhi  ya  maswali  ambayo  nimeulizwa  na  haya  ndiyo  majibu  yake.

1.JE  MALI  ALIYOPEWA  MTU  KABLA  YA  KIFO  CHA   MAREHEMU  NAYO HUHESABIWA   KATIKA  KUGAWANA  MIRATHI.

Yapo  mazingira  ambapo  marehemu  huwa  amempa  mtu/mrithi  mali  kabla  ya  kifo. Mara  nyingi  hii  hujitokeza  kwa  baba au  mama  na  mtoto  ambapo  baba/mama  humpa  mali  mwanae  hata  kabla  ya  kifo. Hampi  ile  mali  kama  amemrithisha  hapana  isipokuwa  anaweza  kumpa  sehemu  ya  mali  pengine  ili ajenge  au  sehemu  ya  shamba  ili  alime    na wengine  huwa  wametoa  vitu  kama  magari  au  hata    nyumba.  

Swali  ni  je  iwapo  mtu  amepewa   vitu  kama  hivi   au  amepewa  kimojawapo  kati  ya  hivi  ni  sawa   vitu  hivi  alivyopewa  kuhesabiwa  wakati  wa  kugawana  mali  za  marehemu  aliyempa  mali  hizo. Jibu  ni  ndiyo, sheria  inasema  iwapo  marehemu  hakuacha  wosia    basi  wakati wa  kugawana  mali  zake   vile  vitu ambavyo  alivitoa  kwa  baadhi  ya  watu/ warithi  yafaa  vihesabiwa  wakati  wa  mgawanyo  wa  mali. 

Sio  kwamba   mtu atanyanganywa   mali  hizo hapana  isipokuwa  aliyekwishapewa  hawezi  kupata  mgao  sawa  na  yule  ambaye  hakuwahi  kupewa  chochote  na   marehemu wakati  wa  uhai.  Ambaye  hakuwahi  kupewa  chochote  yafaa  apate  mgao  zaidi  kuliko yule  aliyekuwa  amepewa  na  marehermu  kabla  ya kifo. 

Isipokuwa   hali  itakuwa  tofauti  iwapo  marehermu  ameacha  wosia.  Ikiwa  marehemu  ameacha  wosia  basi   kila mtu  atapata  kutokana  na wosia  unavyosema  bila  kujali  nani alikuwa  amepewa  kabla  na  nani hakupewa  kabla.  Wosia  utafuatwa  hivyohivyo  ulivyo.

2.  JE  INARUHUSIWA  KUINGIZA  MALI  YA  WANANDOA  KATIKA  MALI  ZA  MIRATHI   ILI  NDUGU  WAZIGAWANE IWAPO  MKE/MME  NDIYE  AMEFARIKI.

Yapo  mazingira  ambapo  mke  anaweza  kumtangulia  mume  katika  mauti  au  mme  anaweza  kumtangulia  mke . Lakini   mpaka  kifo  kinamkuta mmoja   unakuta  tayari  kuna  mali ambazo  zilikuwa  zimechumwa  na  wanandoa  kwa  pamoja   na  hivyo  kuwa  mali  za  familia.  Hapo hapo  unakuta  kuna   warithi  kama  watoto au  ndugu  wengine  na  wanataka  mali  zote  ziingizwe  katika  orodha  ya  mirathi  na  zigawanywe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...