Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda (wa pili kushoto) akimsikiliza Naibu Meya, Songoro Mnyonge wakati akimpa maelezo kuhusu mazingira ya Mto Kiboko uliopo katika Kata ya Tandale wakati wa ziara yake katika Manispaa hiyo, Dar es Salaam jana.
Mkazi wa Mtaa wa Bahi, Jomo Macha akimueleza Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda athari za mafuriko katika Mtaa huo, Kata ya Makumbusho wakati wa ziara ya Meya huyo jana. Wengine ni Watendaji wa Manispaa hiyo na wakazi wa eneo hilo.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda akitoa maelekezo kwa watendaji wa Manispaa hiyo kuhusu kutafuta ufumbuzi wa chemba ya majitaka iliyofurika katika Mtaa wa Balozi Msolomi wakati wa ziara yake. Kulia kwake ni Naibu Meya, Songoro Mnyonge na watendaji wa Manispaa hiyo.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda (mbele) akikagua mto Ng'ombe uliopo eneo la Mwananyamala Kisiwani, wakati wa ziara hiyo Nyuma yake ni Naibu Meya,Songoro Mnyonge.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Eh Mheshimiwa Meya hivi unakwenda kutembelea maeneo ya mafuriko na buti hiyo kali na suti?

    ReplyDelete
  2. sielewi viongozi kwanini hawavai kuendana na matukio...unaendaje kwenye mafuriko na suti na moka?

    ReplyDelete
  3. Ni lini nchi yetu viongozi wataacha kuwa wa kutembelea maafa(aftermath) na kuwa viongozi wa kuzuia maafa kwa kuweka na kutekeleza mipango endelevu?

    ReplyDelete
  4. Hiyo sehemu ina ule uchafu uliokithiri ambao ni vigumu kuelewa kwanini uko hapo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...