Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoa hotuba yake wakati wa ufunguzi wa Kituo cha Taifa Kumbukumbu huko kisasa mjini Dodoma leo.Wapili kushoto ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, watatu kushoto ni Mwenyekiti wa BungeMh. Zungu na kulia ni Waziri wan chi Ofisi ya Rais Utawala BoraMh.George Mkuchika.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifunua kitambaa katika jiwe la msingi kufungua rasmi Kituo cha Taifa Cha Kumbukumbu kilichopo Kisasa mjini Dodoma leo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia jalada la mwaka 1940 ambapo alisoma utendaji kazi wa Babu yake Chifu wa Kabila la Wakwere Mrisho Kikwete wakati huo.Jalada hilo ni moja ya majalada ya zamani yaliyohifadhiwa kutumia teknolojia ya kisasa katika Kituo Cha Taifa Cha Kumbukumbu kilichopo Kisasa mjini Dodoma.Katika hotuba yake wakati wa ufunguzi wa kituo hicho Rais Kikwete ametoa agizo la kuanzishwa maktaba za Viongozi wa kitaifa hususan marais wastaafu ili kuhifadhi vyema historia ya nchi.(picha na Freddy Maro).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hongera sana Serikali kwa kazi nzuri ya kuanzisha kituo hichi muhimu. NASIKITIKA SANA KUONA MAKUMBUSHO YA TAIFA HAIJUI CHOCHOTE MAANA SIJAONA USHIRIKI WAO KATIKA HILI, SIJUI HATAKAMA MKURUGENZI WAO AMESHIRIKI KATIKA JAMBO HILI MUHIMU, HII NI AIBU KWA MAKUMBUSHO YA TAIFA. MH RAIS HEBU TUPIA MACHO YAKO KATIKA SHIRIKA LA MAKUMBUSHO SISI TUNAO PITAPITA HAPO TUMEGUNDUA MATATIZO MAKUBWA SANA, TUMEKUWA TUKITAKA KUJUA NI KWANINI SHIRIKA LINAZIDI KUHARIBIKA TUKAGUNDUA KUWA UONGOZI NA WAFANYAKAZI WAKE NI VITU VIWILI TOFAUTI, UONGOZI UNAJALI MASLAI YAKE ZAIDI BILA KUANGALIA MASLAI YA WAFANYAKAZI WACHINI, INASEMEKANA NI ZAIDI YA MIAKA SITA SASA HAKUNA WALIOPANDISHA VYEO JAPO WATU WAMEJIENDELEZA KIELELIMU. Nazidi kuupongeza mkoa wa Dodoma na Serikali kwa kuanzisha kituo hiki. Mh JAKAYA KIKWETE KABALA UJAONDOKA MADARAKANI PLZZ OKOA MAKUMBUSHO ISIYO NA BODI MIAKA KADHAA SASA NA VIONGOZI WAKE WA KUKAIMU KAHIMU TU.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...