.Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya jijini Windhoek Namibia ambapo walihudhuria sherehe za kuapishwa Rais mpya wa Namibia.

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake akikutana na Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya katika Hoteli ya Safari Court jijini Windhoek Namibia jana.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa pamoja na marais wastaafu Ali Hassan Mwinyi(kulia) na Benjamin William Mkapa(kushoto) katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Hosea Kutako jijini Windhoek Namibia leo.Viongozi hao walihudhuria sherehe za maadhimisho ya miaka 25 ya Uhuru wa Namibia ambapo pia Rais wa awamu ya tatu  wa Namibia Dkt.Hage Geingob aliapishwa katika uwanja wa Independence jijini Windhoek.Chama cha ukombozi cha Namibia SWAPO kilizaliwa nchini Tanzania na kuendesha harakati za ukombozi mpaka mwaka 1990 ambapo nchi hiyo ilipata uhuru. Picha na Freddy Maro.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Wastaafu wetu hawana shida. Mungu Ibariki Tanzania

    ReplyDelete
  2. Nimesoma kwenye Twitter ya Benard Membe kuwa wamekubaliana kuruhusu magari ya tours ya Tanzania kuingia JKIA na ndege za Kenya kuruhusiwa kuendelea na ratiba yake ya kawaida ya safari 42 kwa wiki. Binafsi ninaona bado hatujatatua tatizo hilo kwa njia ya kudumu kwa sababu hilo tatizo litaendelea kuwepo kwenye historia ya nchi yetu kwa kila rais ajaye na kulazimisha kufanyika kwa mazungumzo kama haya mara kwa mara. Suluhisho la kwanza ni kupanua viwanja vyetu vya ndege viwe vyenye hadhi kama vingine kama Jomo Kenyatta ili vivutie mashirika makubwa ya ndege kutoka Ulaya. 2. Tufanye mazungumzo na mashirika makubwa ya ndege ili kuvivutia yaje nchini, pia tupunguze gharama za kutua kwenye hivi viwanja vyetu.....viwanja vyetu vinatoza bei kubwa kuliko vya majirani zetu hasa vya Kenya, tusipopunguze gharama hizi uwezekano ni mdogo wa mashirika makubwa kuja kwetu. ( Kwanini kila kitu nchini kwetu ni ghali kuliko nchi zingine majirani na huduma zetu si za viwango vizuri?
    3. Tuifufue Air Tanzania imilikiwe na Serikali kwa asilimia fulani na hisa zingine ziuzwe kwa wananchi na chache kwa kampuni kubwa yenye kueleweka ( siyo ile ya Oman isiyo hata na ndege moja au sonangol ya China isiyo na uzoefu)
    NB: Tusiwe na mazoea ya kutegemea vya jirani tutaendeea kujiabisha na kupoteza uhuru wote

    ReplyDelete
  3. Anonymous 2 umezungumza mambo ya maana kabisa...Uamuzi huu bado naamini ni wa kukupurupuka kwa haukujadili tatizo na kutoa majawabu ya kudumu wala kugusa ajenda nyingine kubwa kama ya FastJet ku operate Dar- Nairibi kwa bei ya walala hoi.
    Hivi KQ watakuwa wakitulipisha $800 - $1000 kwa safari ya Dar - Nairibi mpaka lini na bila ya Kenya kuruhusu ndege zetu kushiriki na kutoa fursa za ushishindani sawa kibiahsara?

    Kama ni issue ya ya Shuttles hakukuwa na mgogoro lakini wameuanzisha wao na sasa tulivyo malofa tunaona tume win kwa sababu eti wameruhusu tena? sasa tu me win nini?

    ReplyDelete
  4. Wastaafu bado wako fiti kabisa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...