Na Ripota wa Globu ya Jamii,Dar

Sakata la mlinda mlango Juma Kaseja na waajiri wake Yanga limechukua sura mpya baada ya kutakiwa kumalizana nje ya mahakama.

Kesi hiyo ambayo iliendelea leo katika Mahakama ya Kazi baada ya Februari 12 kuahirishwa kutokana na wakili anayemsimia mlinda mlango huyo Samson Mbamba kuunguliwa ofisi yake ambapo nyaraka mbali mbali zikiwemo za Kaseja kuungua na kuomba kupewa upya nyaraka nyingine na kesi hiyo kuendelea leo.

Kesi hiyo ambayo inasuluhishwa na Muheshimiwa Alfred Massey, aliwataka Yanga kumalizana na Kaseja nje ya mahakama na kesi hiyo itaendelea tena Machi 16 saa sita mchana kuangalia iwapo pande zote mbili zimeridhia na kutekeleza masharti waliyopewa.

Katika masharti hayo Kaseja anatakiwa kutaja kiasi gani cha fedha ambacho anaweza kuilipa Yanga huku klabu hiyo nayo ikitakiwa kuangalia kama itaweza kumrudisha kundini Kaseja.

Wakili wa Yanga Frank Chacha, akizungumzia suala hilo alisema "Kuna masharti tumepewa pande zote mbili, masharti ambayo ni siri hatutakiwi kusema kwa vile ni usuluhishi ndio maana hata nyinyi mmezuiwa kuingia kusikiliza, ninachoweza kusema tumeridhia kwa pamoja pande zote kukaa na kumaliza hili suala nje  ya mahakama, na hiyo Machi 16 tutarudi kwa ajili ya kueleza muafaka tuliofikia."alisema Chacha.

Kaseja alipanda kizimbani  kwa mara ya kwanza Februari 12 kwenye Tume ya Usuluhishi na Uamuzi  iliyo chini ya Mahakama ya Kazi kwa lengo la kujibu shtaka la kuvunja mkataba ikiwa ni pamoja na kuilipa Yanga kiasi  cha Sh 340 milioni. Hata hivyo, Kaseja alipelekwa katika hatua ya usuluhihi ili  kujibu kama yuko tayari kulipa fidia  au vipi na kama hakutakuwa na muafaka  kesi hiyo itapelekwa kwenye hatua ya uamuzi ambayo ni sawa na kesi nyingine.

Uongozi wa Yanga  uliingia kwenye uhasama na kipa, Juma Kaseja ‘Tanzania One’ baada ya kumtaka kipa huyo kuwalipa fidia ya Sh340 milioni, baada ya mlinda mlango huyo  kuandika barua Novemba 11 ya kuvunja mkataba na wanajangwani hao, hata hivyo uongozi huo chini ya Yusuf Manji ulipitia barua hiyo ya Kaseja na kumjibu Desemba 15 ikiwa ni mwisho wa dirisha dogo la usajili ikitaka kiasi hicho cha fedha.

Katika majibu ya Yanga kwenda kwa wakili wa Kaseja, Samson Mbamba inataka walipwe ada ya usajili ambayo ni Sh40 milioni pamoja na fidia ya Sh300 milioni ambazo ni gharama za usumbufu wa kuvunja mkataba, kumhudumia na kutunza kiwango chake kwa kipindi chote alichokuwa Yanga.

Kaseja kupitia Kampuni ya Mbamba Advocate iliandika barua ya kuvunja mkataba na klabu hiyo kwa kile ilichoeleza kuwa amekuwa akisugua benchi, pia uongozi wa Yanga umekiuka makubaliano baina ya pande mbili ambazo hadi Januari mwaka huu walitakiwa kummalizia ada yake ya usajili Sh20 milioni, lakini hata hivyo haikufanya hadi alipowasilisha barua ya kuvunja mkataba.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...