Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

Waziri wa Uchukuzi,Samwel Sitta amesema kuwa mabehewa yaliyoingizwa nchini kutokea Kampuni ya M/S Hindusthan Engeneering Industries Limited yapo chini ya kiwango na hivyo wale ambao wamehusika na ukaguzi na kufanya mabehewa hayo yaingizwe nchini watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam mara alipotembelea Shirika la Reli Nchini (TRL),Sitta alisema serikali ikithibitisha waliokagua na kuleta mabehewa hayo watachukuliwa hatua.

“Nchi hii ni masikini hivyo wote waliohusika katika uingiaji wa mabehewa hayo watachukuliwa hatua kutokana na sheria za nchi ikiwa ni pamoja na kusitisha mkataba  huo na hili nitafuatutilia kwa karibu na bodi ya TRL nimeiagiza kufanya hivyo”alisema Sitta.

Alisema kutokana na kuingizwa kwa mabehewa yasio na ubora,wamezuia kuingia tena kwa mabehewa 124 kutokana na mkataba walioingia nao wa kuleta mabebewa hayo.

Sitta alisema hali ya shirika ni nzuri kutokana mapato yake kuongezeka kutokana na watendaji kujipanga katika uendeshaji wa shirika hilo.  
Waziri wa Uchukuzi,Mh. Samwel Sitta (katikati) akizungumza na wandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam leo,wakati alipotembelea Shirika la Reli nchini (TRL). kulia ni Naibu Waziri wa Uchukuzi,Mh. Charles Tizeba na kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi,Monica Mwamunyange,.
Sehemu ya Wanahabari wakimsikiliza Waziri Sitta (hayupo pichani) wakati alipotembelea Shirika la Reli nchini (TRL) jijini Dar leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. The mdudu, mambo yote ya kimaendeleo naomba kuanzia leo yasimamiwe na jwtz na sivinginevyo ili tuwakomoe mafisadi wote. .msicheze na jwtz mtapukutika nyote.

    ReplyDelete
  2. The mdudu we we kiboko nchi iendeshwe na makamanda tena?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...