Naibu waziri wa Kilimo,Chakula na Ushirika Mheshimiwa Godfrey Zambi amezitaka taasisi na mashirika binafsi nchini kubuni mbinu za kuleta mapinduzi katika sekta ya kilimo nchini hususani kuwaendeleza wakulima wadogo ambao idadi yao kubwa wanaishi maeneo ya vijijini. 
 Mheshimiwa Zambi ametoa wito huo jana wakati akifungua kongamano la simu moja la Kilimo Klub lililoandaliwa na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania na alisema kuwa kuna idadi kubwa ya wakulima wanaishi katika umaskini mkubwa na wanafikia hatua ya kuzalisha chakula cha kutosheleza mahitaji yao na familia zao. 
 “Tunataka kuwa na wakulima wanaofanya uzalishaji wenye tija,lakini bahati mbaya wakulima wengi waliopo wanaendesha kilimo kisicho cha kitaalamu huku wakiwa wanakabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo kukosa utaalamu wa kilimo,kukosa taarifa za masoko ya kuuzia mazao yao,kutokuwa na mbimu za biashara ,kutokuwa na sifa za kukopesheka kutoka taasisi za fedha na kuuza mazao yao kwa bei ndogo kutokana na kutokuwa na uwezo wa kuyasafirisha mpaka kwenye sehemu yenye soko kubwa.”Alisema Zambi. 
 Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Rene Meza alisema kuwa ikiwa na mtandao ulioenea kwa asilimia 90 ya Tanzania Vodacom imedhamiria kuwakwamua wakulima vijijini kupitia Kilimo Klub Rene alisema, “Kupitia Kilimo Klub wakulima watanufaika kwa namna mbalimbali na maisha yao kuwa murua kwa kuwa wataweza kupata mikopo rahisi na isiyo na urasimu,wataweza kupata taarifa za masoko na hali ya hewa na kupata ushauri wa kilimo na haya yote yanafanyika kwa njia rahisi kupitia simu zao za mkononi na nina imani wakulima wengi hususani wanaoishi vijijini watabadilika kutoka hali duni na kuwa na maisha bora zaidi” Meza aliongeza kusema kuwa mtandao wa Vodacom umesambaa asilimia 90 ya Tanzania na asilimia 40 ya vituo vyake vya kurusha mawasiliano vipo maeneo ya vijijini na huu ni mmoja ya mkakati wa kampuni wa kusambaza huduma za mawasiliano vijijini na kubuni huduma za kuwarahisishia maisha wakazi wa maeneo hayo ambao wanakabiliwa na changamoto mbalimbali katika maisha yao ya kila siku na nia na uwezo wa kufanya hivyo upo. 
 Alisema hivi sasa maelfu ya wakulima nchini kupitia Kilimo Klub wanaweza kutuma na kupokea fedha kupitia huduma ya M-Pesa na kujiwekea na kupata mikopo nafuu kutoka huduma ya M-Pawa “Huduma hii ya M-Pawa ni tumaini jipya la wakulima vijijini na hadi kufikia sasa tangu ianzishwe mapema mwaka jana maelfu ya wakulima wamejiunga nayo na zaidi ya bilioni 2.5 zimewekwa kama akiba na zaidi ya milioni 500 zimekuwa zikitolewa kwa mkopo kila mwezi. Mpango wa Kilimo Klub ambayo umelenga kubadilisha maisha ya wakulima kuwa murua unaendeshwa kwa ubia kati ya Vodacom Tanzania na taasisi za Connected Farmers Alliance na Techno Serve.
 Naibu Waziri wa Kilimo na Chakula,Mh.Godfrey Zambi(kushoto)akipeana mikono na na Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania, Rene Meza wakati wa kuzindua warsha ya Kilimo Klub iliyoandaliwa na kampuni hiyo iliyolenga kushirikisha wadau mchango wa kampuni hiyo katika kuendeleza sekta ya kilimo kupitia mtandao wake na kujenga msingi wa ushirikiano kati ya wadau hao ili kuendeleza  sekta hii muhimu nchini.Warsha hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam ilishirikisha wadau mbalimbali wa sekta hiyo.
 Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania, Rene Meza(kushoto)akimwelezea jambo Naibu Waziri wa Kilimo na Chakula,Mh.Godfrey Zambi,wakati akiwasili kufungua warsha ya Kilimo Klub iliyoandaliwa na kampuni hiyo iliyolenga kushirikisha wadau mchango wa kampuni hiyo katika kuendeleza sekta ya kilimo kupitia mtandao wake na kujenga msingi wa ushirikiano kati ya wadau hao ili kuendeleza  sekta hii muhimu.Warsha hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam ilishirikisha wadau mbalimbali wa sekta hiyo.
 Naibu Waziri wa Kilimo na Chakula,Mh.Godfrey Zambi akifafanuliwa jambo  na  Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania, Rene Meza(kushoto) kuhusiana na huduma ya M Pawa alipofika kuzindua warsha ya Kilimo Klub iliyoandaliwa na kampuni hiyo iliyolenga kushirikisha wadau mchango wa kampuni hiyo katika kuendeleza sekta ya kilimo kupitia mtandao wake na kujenga msingi wa ushirikiano kati ya wadau hao ili kuendeleza  sekta hii muhimu nchini.Warsha hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam ilishirikisha wadau mbalimbali wa sekta hiyo.
Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania, Rene Meza(kulia) akiteta jambo na Naibu Waziri wa Kilimo na Chakula,Mh.Godfrey Zambi,wakati warsha ya Kilimo Klub iliyoandaliwa na kampuni hiyo iliyolenga kushirikisha wadau mchango wa kampuni hiyo katika kuendeleza sekta ya kilimo kupitia mtandao wake na kujenga msingi wa ushirikiano kati ya wadau hao ili kuendeleza  sekta hii muhimu.Warsha hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam ilishirikisha wadau mbalimbali wa sekta hiyo.
 Naibu Waziri wa Kilimo na Chakula,Mh.Godfrey Zambi,akizungumza na wadau mbalimbali wa Kilimo nchini wakati wa warsha ya Kilimo Klub iliyoandaliwa na Vodacom Tanzania iliyolenga kushirikisha wadau mchango wa kampuni hiyo katika kuendeleza sekta ya kilimo kupitia mtandao wake na kujenga msingi wa ushirikiano kati ya wadau hao ili kuendeleza  sekta hii muhimu.Warsha hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wadau walioshiriki warsha ya Kilimo Klub iliyoandaliwa na Vodacom Tanzania,wakijadiliana jambo wakati wa warsha hiyo iliyolenga kushirikisha wadau mchango wa kampuni hiyo katika kuendeleza sekta ya kilimo kupitia mtandao wake na kujenga msingi wa ushirikiano kati ya wadau hao ili kuendeleza  sekta hii muhimu nchini.Warsha hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam ilishirikisha wadau mbalimbali wa sekta hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...