Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Sehemu ya pili
    Takwimu zinaonyesha, ili uchumi ukue, tunahitaji sekta imara ya viwanda. Na hii ni kwasababu, viwanda vinaufanisi zaidi ukilinganisha na kilimo. Kwa uhalisia swala si kuchagua kati ya kilimo na viwanda, bali kufikiria kilimo bila kufikiria viwanda. Kwa Tanzania viwanda vinaweza kutumia rasilimali zetu (kwa mfano viwanda vya nguo kutumia pamba; au viwanda vya unga au bidhaa ya plastiki kutokana na zao la mahindi n.k). Uwepo wa viwanda hivi utaongeza mahitaji (demand) ya mazao yetu, jambo litakalosababisha bei za mazao na uzalishaji wake viongezeke hivyo kuwafanya wakulima wetu wapate faida kutokana na kilimo, wakati huo huo nchi ikiongeza uzalishaji wa mazao ya kilimo pamoja na bidhaa za viwandani. Badaya ya kudhamiria kuuza mazao ya kilimo nje ambayo mara nyingi yana bei ndogo kwa kutoongezwa thamani, bidhaa za viwandani zitaongeza pato la taifa kwa kuuza bidhaa ambazo zina thamani zaidi.

    Jambo jingine ambalo watoa takwimu na wachumi wanasahau kulisisitiza ni kuwa, ijapokuwa ni kweli kuwa zaidi ya asilimia 70 ya Watanzania wanaofanya kazi wameajiriwa kwenye sekta ya kilimo, kulingana na takwimu za 2014, takriban asilimia 50 ya Watanzania wana umri wa miaka chini ya 18. Swali ni kuwa, tunawaandalia uchumi gani kizazi hiki kinachoingia kwenye soko la ajira katika miaka michache ijayo? Je tunataka waingie kwenye kilimo? Tukumbuke kizazi hiki asilimia kubwa watajua kusoma na kuandika, watamaliza elimu ya msingi, sekondari na kadhali. Nadhani kusema Tanzania ijayo iwe ya kilimo pekee (kwa maana ya kilimo kama end result) sio njia nzuri zaidi ya kusaidia kuondoa umasikini na kuleta utajiri katika nchi yetu.

    Napenda kusema, japokuwa kilimo ni muhimu, hasa kwa wakati wa sasa, viwanda ni muhimu zaidi tuendako. Tukianzisha uchumi wa viwanda sahihi, tutachechemua sekta ya kilimo kwa kuongeza mahitaji (demand) na Tanzania ya sasa na ya baadaye itaweza kuhimili vizuri zaidi ushindani kutoka nje na kuchukua fursa za uchumi unaokuwa ndani ya Tanzania, majirani zetu na Afrika kwa ujumla.

    Kwanini viwanda leo? Moja ya shida kubwa inayoathiri viwanda vya Tanzania leo na pia inakatisha tamaa uwekezaji kwenye sekta hiyo, ni bei kubwa ya nishati ya umeme na pia kutokupatikana kwa umeme wa uhakika. Uwepo wa gesi asilia, zaidi ya kuongeza mapato kwa serikali, itawezesha wanaofua umeme kuzalisha umeme wa bei nafuu na wa uhakika. Vilevile, wale walio mbali na mfumo wa usambazaji wa umeme wa Tanesco wataweza kuzalisha kwa kufunga mitambo ya uzalishani umeme hukohuko waliko kwani gasi ni fueli inayosafirishika. Vyote hivi vitapunguza ugumu wa maendelea katika sekta ya viwanda, na tunaweza kufaidika vyema kama serikali yetu na watu wake tutafanya kazi kwa bidii kuchangamkia fursa zinazojitokeza kutokana na upatikanaji wa gesi asilia nchini Tanzania.

    Mungu ibariki Tanzania

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...