Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Rajabu Gamaha akizungumza wakati wa mkutano kati yake na Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje ya China, Balozi Liu Songtian  (hayupo pichani). Balozi Liu na ujumbe wake wapo nchini kwa ajili ya kufuatilia masuala ya uwekezaji na maendeleo ya viwanda Tanzania ikiwa ni miongoni mwa nchi tatu za Afrika zilizochaguliwa na China kwa ajili ya kuwa mfano katika uwekezaji na maendeleo ya viwanda. Nchi zingine ni Ethiopia na Kenya. Wengine katika picha ni Balozi Mbelwa Kairuki (kushoto kwa Bal. Gamaha), Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia, Mhe. Abdulrahman Shimbo (mwenye tai nyekundu), Balozi wa Tanzania nchini China na Kanali Mstaafu Joseph Simbakalia (kulia), Mkurugenzi Mkuu wa EPZA.
Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje ya China, Balozi Liu Songtian akizungumza wakati wa mkutano kati yake na Balozi Gamaha na ujumbe wake. Kulia ni Balozi wa China hapa nchini, Mhe. Lu Yoqing.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...