Mfuko
wa Maendeleo ya Jamii TASAF unaendelea kutoa mafunzo kwa waandishi wa habari
ili waweze kutumia vyombo vya habari vilivyoko
kwenye maeneo yao kutangaza habari za Mpango wa kunusuru kaya masikini unaoratibiwa
naMfuko huo.
Akifungua
mafunzo hayo yanayoendeshwa kwa utaratibu wa Kikao Kazi Mkurugenzi Mtendajiwa
TASAF Bwana Ladislaus Mwamanga amesema kazi ya kutokomeza umaskini nchini inahitaji
ushiriki wa wadau mbalimbali vikiwemo vyombo vya habari.
Bwana
Mwamanga amesema tangu TASAF ianze kutekeleza Mpango wa kunusuru kaya masikini kumekuwa
na mafanikio makubwa hususani katika maeneo ya walengwa ambao wameanza kuboresha
maisha yao na katika baadhi ya maeneo walengwa wameanza kukuza shughuli za kiuchumi
huku wengine wakiweza kuhudumia kaya zaokinyume na hali ilivyokuwa huko nyuma.
Amewasihi
waandishi wa habari kuwatembelea walengwa wa Mpango huo ili kuona namna walengwa
hao wanavyonufaika na Mpango huo wa uhawilishaji fedha na kisha kutangaza mafanikio
yaliyokwisha patikana huku akisisitiza kuwa hata pale penye changamoto zionyeshwe
ili marekebisho yafanyike kwa manufaa ya walengwa
Zifuatazo
ni baadhi ya picha za washiriki wa kikao kazi hicho kilichofanyika kwenye ukumbi
wa mikutano wa Chuo kikuu Huria Mjini Mtwara.
Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Mtwara
Bwana RenatusMongogwela (mwenye shati nyeupe)akizungumza na ujumbe wa TASAF
ulioongozwa na Mkurugenzi mtendaji Ladislaus Mwamangawa, kwanza
kushoto kwa kaimu katibu tawala.
Mkurugenzi Mtendajiwa
TASAF Bwana Ladislaus Mwamanga aliyesimama akifungua kikao kazi cha watendajiwa
TASAF kutoka maeneo ya utekelezaji wa Mpango wa kunusuru kaya
maskini na waandishi wa habari wa mikoa ya Mtwara na Lindi (hawapopichani)
Washiriki wa kikao kazi
cha watendaji wa TASAF
na waandishi wa habari kutoka mikoa ya Mtwara na Lindi wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa
TASAF Bwana Ladislaus Mwamanga(hayupo pichani).
Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF bwana
Ladislaus Mwamanga akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watendaji wa TASAF
makao makuu baada ya kufungua kikao kazi cha waandishi wa habari wa mikoa ya Mtwara na Lindi.
Mkurugenzi Mtendajiwa TASAF Bwana
Ladislaus Mwamanga akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watendaji wa TASAF
makao makuu baada ya kufungua kikao kazi cha waandishi wa habari wa mikoa ya Mtwara na Lindi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...