Hivi ndivyo hali ilivyo katika maeneo mengi hapa jijini Dar,kutoka na Mvua zinazoendelea kushesha.Kwa Mujibu wa Mamlaka ya Hali ya hewa nchini,inaeleza kwamba Vipindi vya mvua hii inayozidi milimeta 50 ndani ya masaa 24 itaendelea kuwepo katika baadhi ya maeneo ya ukanda wa pwani wa nchi ikihusisha mikoa ya Lindi, Mtwara, Pwani, Dar es Salaam pamoja na kisiwa cha Unguja,hiyo ni kutokana na kuwepo na kuimarika kwa ukanda wa mvua (Inter Tropical Convergency Zone –ITCZ) katika maeneo hayo.
Barabarani huko nako mambo ni kama hivi.
Huku mitaani ndio usiseme,maana njia zote zimejaa maji.
Mitaro inaonekana haipo au imeziba sehemu nyingine.
ReplyDeleteUjenzi holela/mipango miji haikupewa kipaumbele kwenye mipango kazi.
ReplyDelete