WAZIRI wa Ujenzi Dkt. John Magufuli ametoa siku 14, kwa
Wakala wa Majengo ya Serikali (TBA), kuanza ukarabati wa
ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Siha na Moshi baada ya kubainika
majengo hayo kujengwa chini ya kiwango.
Dkt. Magufuli pia ameagiza aliyekuwa meneja wa TBA Mkoa
wa Kilimanjaro, Paul Ndossa kusimamishwa kazi mahali alipo
ili arejee kujibu tuhuma na kuwajibishwa kwa mujibu wa sheria.
Waziri huyo alitoa agizo hilo wakati akikagua jengo la mkuu wa
Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro baada ya kupewa taarifa za
jengo hilo kujengwa chini ya kiwango hali iliyosababisha
shughuli za mkuu wa Wilaya ya Siha kuhamishiwa kwenye ofisi
za maji za halamashauri hiyo.
Kwa upande wake Ofisa Mtendaji mkuu wa TBA Elius
Mwakalinga alisema wakala hao wanasikitishwa na kasoro za
kiufundi zilizojitokeza katika jengo hilo na watawachukulia
hatua wote waliohusika katika kuchangia majengo hayo kuwa
chini ya kiwango.
Mwakalinga amesema tayari TBA imefanya tathmini ya
gharama za ukarabati wa jengo la Wilaya ya Siha ambao
utafanyika katika kipindi cha wiki 18 na kugharimu shilingi
milioni 50.
Majengo ya ofisi za wakuu wa Wilaya za Siha na Moshi
yalijengwa kwa usimamizi wa TBA ambapo wahusika
walishindwa kuyatumia wakihofia usalama wao baada ya kuona
dosari.
Hongera sana Mh Dkt Mangufuli kwa utendaji wako wa kazi. Chakushangaza nikwamba mpaka majengo haya yanakamilika na kukabidhiwa katika kiwango cha chini, Eng wa wilaya,Mh DC, Katibu Tawala,Waheshimiwa madiwani walikuwa wapi?? Ingependeza sana kama na wenyewe wangewajibishwa. Mali za serikali nilazima tuwe na uchungu nazo,nikodi za walala hoi.
ReplyDelete