Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania imeeleza kuguswa na tukio la mvua kubwa iliyonyesha wilayani Kahama mkoani Shinyanga ambayo imesababisha vifo vya watu 42 na wengine mamia kujeruhiwa na kuacha familia nyingi zikiwa hazina makazi na kuanzia leo imeanza kampeni ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia wahanga wa tukio hilo.

Akiongea na waandishi wa habari leo,Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia amesema anawaomba watanzania wote wanaotaka kuchangia wahanga hao kutuma fedha zao kwenye namba maalumu ya kupokea msaada ya kusaidia majanga mbalimbali ya 155990.

“Tukiwa kama kampuni ya mawasiliano tumeguswa na tukio hili na tunawapa pole waathirika wote na tunaungana na wakazi wa kahama kwa janga hili tutatoa mchango wetu wa hali na mali kwa kupitia kitengo chetu cha kusaidia jamii cha Vodacom Foundation na tunawaomba watanzania wote wenye nia ya kuwasaidia wahanga watume michango yao na tutahakikisha tunaifikisha sehemu inayohusika kuwasaidia wenzetu ambao wako katika mazingira magumu na wanahitaji msaada wa haraka”.

Alisema kupitia njia hii ya namba maalumu ya”Red Alert” 155990 ya kuchangisha fedha imewahi kurahishisha uchangishaji wa fedha kwa waathirika wa matukio yaliyotokea siku za nyuma na kuathiri wananchi moja ya matukio hayo ni milipuko ya mabomu ya Mbagala na Gongo la mboto jijini Dar es Salaam na aliwahimiza wananchi kuitumia kama njia rahisi ya uchangiaji.

Jinsi ya kuchangia ni rahisi sana unachotakiwa kufanya unaponyeza *150*00# alafu unachagua namba 4 yaani Lipa kwa M PESA baada ya hapo utachagua namba 4 tena yaani weka namba ya kampuni unaweka namba 155990 alafu unaweka namba ya kumbukumbu ambayo ni namba yako ya simu baada ya hapo unaweka kiasi cha fedha unachotaka kuchangia.
Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia akionesha namba ya Red Alert ambayo watanzania wote wenye nia ya kuwasaidia wahanga watume michango yao kwenye hiyo namba.Jinsi ya kutuma ponyeza *150*00# alafu unachagua namba 4 yaani Lipa kwa M PESA baada ya hapo utachagua namba 4 tena yaani weka namba ya kampuni unaweka namba 155990 alafu unaweka namba ya kumbukumbu ambayo ni namba yako ya simu baada ya hapo unaweka kiasi cha fedha unachotaka kuchangia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...