WAKATI zimebaki siku chache kwa timu za waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari kuanza kinyang'anyiro cha kuwania ubingwa wa Kombe la NSSF, timu kongwe ya TBC imepokea vifaa vya michezo kutoka Kampuni ya Isere Sports kwa ajili ya michuano hiyo.

Katibu wa timu ya TBC, Jesse John alisema vikosi vyake vinajifua usiku na mchana kuhakikisha ukongwe wao katika fani ya habari unaonekana kwa ushindi wa uwanjani.

"Tunaishukuru Kampuni ya Isere kwa kutusaidia vifaa vya michezo vitakavyokuwa chachu ya kujituma kwetu kuhakikisha tunachukua ubingwa mwaka huu" alisema Jesse John ambaye ni kipa namba moja wa timu hiyo.

Mkurugenzi wa Masoko wa Isere Soprts, Abbas Isere alisema kampuni hiyo itaendelea kushirikiana na wadau wa michezo  na kuwa mstari wa mbele kutoa vifaa vya michezo kwa wanamichezo na pia iko mbioni kuanzisha bonanza maalum kwa wapenda michezo hapo baadaye.

Alisema Isere Sports ambayo ni familia ya wanamichezo inaonelea kuwa ikisaidia kuinua michezo nchini tkaokoa maisha ya vijana watanzania ambao badala ya kukaa vijiweni na kujiingiza kwenye biashara haramu wanaingia viwanjani kufanya mazoezi ili kuiweka mili yao fiti.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Nakuona my mate Jesse John, ungali unaendeleza juhudi zako za dhati kwa ari na nia moja kabisa ili kuhakikisha suala zima la ki-sport halitetereki. Nakuaminia asilimia zote khususan unapokuwa langoni unadhibiti vilivyo angle zote hakipenyi kitu. Keep it up na kila la kheri kwa timu yako nzima tukitarajia ushindi mkubwa TBC.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...