Kampuni ya Tanzania Distilleries LTD (TDL),imechangia kiasi cha sh.milioni 10 kwa harakati ya Imetosha inayopiga vita mauaji ya watu wenye Ualbino,ambayo itafanya matembezi ya hisani machi 29 mwaka huu yatakayofanyika kuanzia katika viwanja vya Biafra na kuishia katika Viwanja vya Leaders Klabu,Kinondoni jijjni Dar es Salaam.
Akizunguma na waandishi wa habari wakati kutangaza kutoa mchango huo,Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo,David Mgwassa amesema kupinga mauaji ya watu wenye ulemavu ni jukumu la kila mtanzania,hivyo TDL kama watanzania wameona umuhimu kuchangia harakati hizo,kwani hata sifa mbaya zinazopatikana nje ya nchi hazilengi mtu mmoja au kundi fulani.
Amesema watu wengine wajitokeze kuunga mkono harakati hizo ili kuwa sehemu ya watu ambao wanaguswa na suala la mauji ya watu wenye ualbino.
Matembezi hayo yataongozwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mathias Chikawe ambapo ujumbe wa serikali utatolewa katika harakati zinazoendelea za kukomesha mauaji ya watu hao wenye Ualbino.
Akizungumzia Matembezi hayo,Balozi wa Harakati ya Imetosha,Henry Mdimu amesema matembezi hayo hayalengi kukusanya fedha wanachohitaji ni watu washiriki matembezi hayo.
mdimu amesema kuwa harakati hiyo ni ya kutoa elimu katika mikoa ambayo mauji ya watu wenye ualbino ili kuweza kubadilisha hali hiyo na isiendelee kuwepo.
"Hatulengi masuala ya fedha tunachotaka wananchi wafikishiwe elimu na watu wanaofanya hivyo washindwe kufanya kutokana na elimu iliyotolewa kuanzia katika familia"amesma Mdimu.
Amesema harakati hizo zimetokana na nguvu ya wadau ambao wamejitolea nguvu zao katika kuweza kukomesha mauaji ya watu wenye Ualbino hapa nchini.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Tanzania Distilleries LTD,David Mgwassa akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kutangaza kuchangia kiasi cha shilingi milioni 10 kwa Mfuko wa Imetosha Foundation.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Tanzania Distilleries LTD,David Mgwassa (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kutangaza kuchangia kiasi cha shilingi milioni 10 kwa Mfuko wa Imetosha Foundation.Kushoto ni Balozi wa Harakati ya Imetosha,Henry Mdimu na kulia ni Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network,Joachim Mushi.
Balozi wa Harakati ya Imetosha,Henry Mdimu akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kwenye ukumbi wa Idara ya habari MAELEZO jijini Dar es salaam leo,wakati wa kutangaza matembezi ya hisani yatakayofanyika Machi 29 kwenye Viwanja vya Leaders Club,jijini Dar es salaam na kuongozwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mh. Mathius Chikawe.Wengine pichani toka kulia ni Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network,Joachim Mushi,Katibu wa Harakati ya Imetosha,Salome Gregory pamoja na Mwanamuziki Mkongwe nchini,Jhiko Manyika "Jhikoman".
Sehemu ya Wajumbe wa Harakati ya Imetosha waliofika kwenye Mkutano na Waandishi wa habari kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO jijini Dar es salaam,wakiwa kwenye picha ya pamoja.
Sehemu ya Wajumbe wa Harakati ya Imetosha waliofika kwenye Mkutano na Waandishi wa habari kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO jijini Dar es salaam,wakiwa kwenye picha ya pamoja.
Michango pia itumike kuboresha baadhi ya makazi duni wanayokaa watu wenye ulemavu wa ngozi.
ReplyDeletePesa nyingi zinakusanywa mpaka sasa ni 20M ziwekwe wazi kuanzia matumizi mpaka michango na wakati huohuo zisitumike kuandaa matamasha then ikaishia kutoa matamko mjini wakati inatakiwa kufanyika vijijini mahali palipo na elimu duni, Ushauri tu haya matembezi yafanyike popote pale ndani ya kanda ya ziwa badala ya DSM lasivyo tutakuwa tunatwanga maji kwenye kinu.
ReplyDeleteJamani hii ni sehemu watu kupata ualaji. Hakuna sehemu inatosha imeweka malengo na mchanganuo wa nini kitatumika au itasadiaje waathirika. Kama mdau mmoja alivyosema hapo juu hizi press conference na matembezi zifanyike kanda ya ziwa kwani huko ndio haya matukio kila siku yanatokea na mengi hayaripotiwi na vyombo vya habari.
ReplyDeleteHili ni dili kama madili mengine yote yaliyopita mf. BRN, Kilimo kwanza n.k hapa watu wanapiga hela hamna kitachofanyika
ReplyDeleteMdau wa kwanza nafikiri hiyo nayo point. Ni kweli hawa ndugu wanahitaji pia mazingira bora ya kuishi ili kuwazuia kuvamiwa piwa. Pesa hizo zingesaidia kutoa elimu sawa lakini waangalie pia na makazi yao kuboresha, au serikali iwatafutie sehemu jirani na watu ili iwe ulinzi pia. Serikali ikiamua inaweza na watanzania ni watu wema sana wanaweza kusaidia hilo naamini.
ReplyDeleteNidhahiri kuwa janga hili limewagusa watanzania wengi emotionally na obviously response ya watu binafsi, mashirika na makampuni imekuwa nzuri.
ReplyDeleteNiungane na wachangiaji hapo juu na kuhoji hii organization ina mipango gani kusaidia kupunguza km sio kutokomeza tatizo hili,or is this going to be just a mere campaign na ndio basi?
Hizi ni kampeni za uchangishaji hela ila hakuna plan yeyote ya kuwa nini kitafanyika baada ya hela hizo kupatikana. Hadi sasa million 200 zimepatikana bado tunapiga press conference tu. Tuende Sumbawanga/kanda yote ya ziwa. Kama wadau wote walivyosema hapo juu hii inaonekana ni ualaji tu kama mambo mengine.
ReplyDelete