Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mhe Zitto Zuberi Kabwe (pichani) usiku huu ametangaza rasmi Bungeni Dodoma kuachia kiti hicho alichokipata kupitia CHADEMA.
Mhe. Kabwe ametangaza kung'atuka nafasi hiyo baada ya Mwenyekiti wa Bunge Mhe Mussa Hassan Zungu Kumruhusu kutoa kauli binafsi mara baada ya wabunge kumaliza kupitia vifungu vya sheria ya Maafa ambayo hata hivyo haikupitishwa kwa kutotimia akidi ya wabunge ambao nusu yao hawakuwepo ukumbini.
 Juu Mheshimiwa Zitto Kabwe na wabunge wengine wakitoka Bungeni mjini Dodoma leo. Chini akiwa na Mbunge wa Ludewa Mhe. Deo Filikunjombe (kuhoto) na Mbunge mwingine
Mhe Zungu alimtakia kila la heri Mbunge huyo machachari ambaye amesema ameamua kuachia ngazi baada ya chama chake kumfukuza. Hata hivyo alimalizia kwa kusema kwamba  Mungu akipenda atakuwa nao tena mwezi Novemba mwaka huu. Hakufafanua. Video ya tamko lake hilo hii hapa...
Mhe.Zitto Kabwe akiongea na waandishi wa Habari usiku huu mara baada ya Kuwaaga Wabunge Baada ya kuwasomea barua aliyomwandikia Mhe.Spika ya Kung'atuka Ubunge baada ya kuvuliwa Uanachama na chama chake cha CHADEMA
Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA ambaye pia ni msemaji wa katiba na sheria wa kambi ya upinzani Bungeni Mhe.Tundu Lissu (wa pili kushoto) akiongea  na wabunge wenzake wakati akitoka katika kikao leo jioni Mara baada ya Zitto Kabwe kung'atuka Ubunge. Wengine pichani kutoka kushoto ni Mhe. Engineer Christopher   Chizza, Mhe.Mchungaji Peter Msigwa na Mhe. Ismail Aden Ragge. Picha zote na Deusdedit Moshi wa Globu ya Jamii Kanda ya Kati

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Michango yako Mh. Zitto kwa taifu letu ni kubwa sana!

    Naomba, nipendekeze kwa Mh. Rais kama ataweza kumteua ZK kama Mbunge wa Kuteuliwa [Nominated MP] kulingana na Ibara 46(1) ya Katiba letu tukufu ya mwaka 1977.

    Tujikumbushe kwamba, hivi sasa tuna wabunge wa kuteuliwa nane wakiwemo:

    *Zakia Meghji [2010]
    *Prof. Makame Mbarawa [2010]
    *Shamsi Vuai Nahodha [2010]
    *Saada Salum [2012]
    *Janet Mbene [2012]
    *Prof. Sospeter Muhongo [2012]
    *James Mbatia [2012]
    *Dr Asha Migiro [2013]

    Kwa hiyo, kabla ya Bunge la 10 kuvunjika; Mh. Rais anaweza kuwateua Mwanamke na Mwanaume mmoja!

    Wadau mnasemaje? Nawasilisha hoja..

    ReplyDelete
  2. Naomba nijisahihishe:

    Nilikosea hapo juu. Ibara sahihi ni 66(1)(e) na sio 46(1).

    Samahani kwa usumbufu.

    http://www.judiciary.go.tz/downloads/constitution.pdf

    ReplyDelete
  3. Nakuhunga Mkono Ndugu ALI... Kwenye katiba mpya kuna mabadiliko ya kifungu hiki kwani.Nchi kama Uingereza kifungu hiki kimewekwa kuwa kama unatoka utatolewa kwenye chama unakuwa huru. Na unaweza kuwa bado mbunge kwani umechaguliwa na wananchi kuwawakilisha na kwenye demokrasia nafikiri kitu kama hiki kinatakiwa kupewa kipaumbele sana.

    ReplyDelete
  4. Hili ni jembe...pumzika jembe but i know you will come back strongly like an injured tiger!!bongo watu kama nyie mko wachache sana na mnapigwa vita...hongera jembe umeondoka kishujaa.Big up!!
    Mdau wa Oxford,UK,

    ReplyDelete
  5. MIMI NAMSHAURI MH. ZZK AGOMBEE TENA UBUNGE KATIKA LILE JIMBO LAKE KUPITIA CHA CHOCHOTE KINGINE LAKINI ISIWE C.C.M. AU CHADEMA NA ATAPITA TU KWASABABU KAZI YA KIJANA HUYU TUMEIONA.

    ReplyDelete
  6. Wanapashwa kuacha kuchagua watumishi wa serikali na wizara kutoka kwa wabunge.

    ReplyDelete
  7. Huu ndiyo unaitwa ukomavu wa kisiasa.

    Mbunge aliyefukuzwa ubunge kukubali kungatuka ubunge na pia chama kilichomvua uanachama kuhakikisha kuwa katiba,kanuni na taratibu za chama zinafuatwa.

    Hongereni wadau wote yaani mbunge ambaye ni mwanachama yaliyefukuzwa na chama cha CHADEMA kwa kuzingatia taratibu, kanuni na katiba mlizojiwekea.

    Mdau
    Diaspora

    ReplyDelete
  8. hiyo poa kabisa. JK Changamka bwana!

    ReplyDelete
  9. Yataka moyo na unyenyekevu, kufukuzwa na kuja mbele ya wabunge wenzako kuaga. Huo ni moyo wa kishujaa sana. Hongera, na mpende Mungu atakujalia tena unayohitaji hapo baadaye. Bye MH ZZK

    ReplyDelete
  10. Ni kweli kabisa

    ReplyDelete
  11. Kuwa rais wa Tz ni rahisi kuliko kuwa mwenyekiti wa Chadema. vita yake kubwa kuliko kupiga kampeni ya uraisi.

    ReplyDelete
  12. Napenda kukupinga kwa nguvu zote mchangiaji wa kwanza ETI ndg Zitto arudishwe bungeni kama mbunge wa kuteuliwa..
    ZZK ni jembe la nguvu halihitaji hisani ya rais ili aweze kurudi bungeni, wananchi wa jimboni kwake wanamtaka na watanzania wengi wanampenda pia kwa hio he will be back bungeni baada ya kuchaguliwa na wananchi tena hahitaji hisani ya rais kumchagua hao wote uliowaweka hapo wamo bungeni kwa vile hawachaguliki na kuwalinganisha na jembe langu ZZK please give him a break.. muache apumzike ajipange vizuri Chadema sio baba yake au mama yake..nawakilisha.

    ReplyDelete
  13. Asante Bw. Ally Ahmed kwa maoni yako. Naomba nikuulize: Kweli ZK ataweza kurudi tena ndani ya Bunge la 10? Hawezi kwasababu hatutakuwa na uchaguzi mdogo [by-election] kulingana na Elections Act of 1985 [Sheria ya Uchaguzi ya mwaka 1985]. Ndio maana, pia, hatuna uchaguzi mdogo jimboni Mbinga Magharibi kwa Marehemu Capt. Komba.

    Ukitaka ZK arudi ndani ya Bunge hili kabla haijavunjwa mwezi [nadhani] July; ni njia mmoja tu: Kwa kuteuliwa! Rais anaweza kumteua; na vile vile ZK anweza kukataa uteuzi kama anataka kupumzika kidogo kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka. Ila, akikubali, itabidi ajiunge na chama cha siasa kingine ili aweze kuteuliwa kwa mujibu wa katiba yetu kinachotuongoza hivi sasa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...