Mratibu wa mradi wa ruzuku kwa waandishi wa habari wa mfuko wa waandishi wa habari nchini (TMF) Danstan Kamanzi akizungumza jana mjini Dodoma na kikundi cha waandishi wa habari wanaoandika habari za wasiosikika (Sauti ya mnyonge) kwenye mafunzo ya siku tano ya kuandika habari za mitandao ya jamii yanayofanyika Dodoma hotel.
Miongoni mwa waandishi wa habari 17 wa kikundi cha waandishi wa habari wanaoandika habari za wasiosikika (Sauti ya mnyonge) wakiwa mjini Dodoma kwenye mafunzo ya siku tano ya kujengewa uwezo wa kuandika habari kwa njia ya mitandoa ya kijamii (social media) yaliyoanza jana.
Mratibu wa mradi wa ruzuku kwa wanaandishi wa habari wa mfuko wa waandishi wa habari nchini (TMF) Danstan Kamanzi (kushoto) akimkabidhi mjini Dodoma, Mwenyekiti wa kikundi cha waandishi wa habari wanaoandika habari za wasiosikika (Sauti ya mnyonge) Ramadhan Msangi moja kati ya kompyuta ndogo (tablet) jana kwa ajili ya kufanya shughuli za kikundi hicho.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...