Mhariri mkuu wa Bongo5 Bw. Fredrick Bundara (kushoto) akiwa pamoja na Mhariri msaidizi, Sandu George wakizungumza leo na waandishi wa habari katika uzinduzi wa Tuzo za watu 2015.
Kampuni ya Bongo5 Media Group, imezindua msimu mpya na wa pili wa Tuzo za Watu Tanzania zilizoanzishwa mwaka jana ili kuwatuza watu kwenye sekta ya burudani na habari wanaofanya vizuri.
Akiongea kwenye mkutano na waandishi wa habari leo, mhariri mkuu wa mtandao wa Bongo5, Fredrick Bundala amesema tuzo za mwaka huu zimeboreshwa zaidi kwa kuongeza vipengele vitatu vipya.
“Mwaka huu tuzo zimeongezewa nguvu zaidi. Kutoka vipengele 11 tulivyokuwa navyo mwaka jana hadi vipengele 1. Mwaka huu tumeongeza vipengele vitatu muhimu,” amesema Bundala.
Amevitaja vipengele vilivyoongezeka kuwa ni pamoja na muongozaji wa filamu anayependwa, tovuti/blogu inayopendwa na mfadhili maarufu anayependwa.
“Kwenye jamii yetu kuna watu maarufu ambao wamekuwa mstari wa mbele kusaidia jamii hususan watu wasio na uwezo ama wanaoshi katika mazingira magumu. Tumeona ni muhimu pia kuwatambua watu hawa ambao huamua kujinyima na kugawana kile wanachokipata ili kuwasaidia watu wanaohitaji msaada,” ameongeza.
Amesema zoezi la kuanza kupendekeza majina ya washiriki limeanza rasmi Alhamis hii ambapo wananchi wanaweza kuwapendekeza kupitia website ya www.tuzozetu.com ama kwa njia ya ujumbe mfupi wa simu kwa kuandika neno TZW, code ya kila kipengele na jina la anayependekezwa kwenda 15678.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...