Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Eng. Patrick
Mfugale amesema hakuna ufisadi wowote wala malipo tata yaliyofanywa
na wizara ya ujenzi kwa makandarasi na wahandisi washauri katika bajeti
ya mwaka 2011/2012.
Eng. Mfugale amesema fedha zote zilizotengwa kwa ajili ya kasma maalum
ya ujenzi wa miradi ya barabara nchini kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni 252
kilitumika kulipa madai ya Makandarasi na Wahandisi washauri.
Eng. Mfugale amesisitiza kuwa Serikali inajenga barabara kwa kuzingatia
vipaumbele vya maendeleeo na hulipa makandarasi na wahandisi
washauri ili kuwezesha kazi hizo kufanyika kwa wakati na kwa kuzingatia
mikataba.
Eng. Mfugale ametoa ufafanuzi huo kufuatia baadhi ya vyombo vya habari
kunukuliwa kuwa kumekuwa na ubadhirifu ,au matumizi tata katika malipo
ya wakandarasi Wizara ya Ujenzi na kusisitiza kuwa suala hilo
lilishajadiliwa na kupatiwa ufumbuzi na Kamati ya Bunge ya Hesabu za
Serikali (PAC), katika kikao chake cha Agosti 22 mwaka 2013.
Amewataka watumishi wa TANROADS kote nchini kuendelea na shughuli
zao za ujenzi na usimamizi wa barabara bila kuvunjika moyo kwani
hakuna ubadhirifu wowote.
Zaidi ya km 35,000 za barabara hapa nchini zinasimamiwa na
TANROADS kupitia mameneja wake katika mikao 25 nchini kote ambapo
takriban KM 11,154 zinajengwa kwa kiwango cha lami katika kipindi hiki.
Jamani fukieni mashimo kupunguza ajali kama iliyotokea Mafinga leo...hii ajali sio uzembe wa madereva..haya mshimo yamekuwa kwa muda mrefu. Viongozi wanapita...mabosi wakubwa tu wanapita jamani hii ni barabara kuu inayotegemewa sana hapa nchini mwetu...Tafadhali zingatieni hili..na kulifanyia kazi..kama yale mashimo yangezibwa hii ajali ingeweza kuepukika
ReplyDelete