Baadhi ya watalaam kutoka Kampuni ya Elektro Merl ya nchini Austria ambao walileta na kufunga makontena ya umeme wa jua pamoja na mfumo wa usambazaji umeme kwa vijiji 10 vilivyo mbali na gridi ya taifa, pamoja na baadhi ya wataalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini, wakikagua moja ya makontena ya umeme wa jua katika Kijiji cha Lobilo, wilaya ya Kongwa, mkoani Dodoma hivi karibuni.
Baadhi ya nyumba za wananchi katika Vijiji vya Lobilo na Silale, wilayani Kongwa, mkoa wa Dodoma, zilizounganishiwa huduma ya umeme wa jua kupitia makontena maalum.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Hizi nyumba zinaweza kuboreshwa zaidi na kuwekwa kwenye viwango vya karne ya 21 vtakavyompatia mkazi nyumba ya kudumu inayokidhi ubora na afya ya mkazi.

    ReplyDelete
  2. Umeme huu wa jua ni maendeleo, lakini wananchi wahamasishwe kujenga nyumba bora kwa manufaa yao wenyewe.

    ReplyDelete
  3. Hongeren.wizara

    ReplyDelete
  4. Hongereni Wizara husika. Nadhani ni maendeleo mazuri vijijini na pia itahamasisha nguvu ya uzalishaji wa bidhaa kuongezeka na khasa kwa vijana pia itawaondolea ile tamaa ya kukimbilia mijini, si kwa ajili ya kuona umeme, la khasha! Bali naamini wataweza kujibunia biashara na shughuli mbali mbali kwa msaada mkubwa wa upatikanaji wa umeme huo. Na kama alivyoeleza mdau hapo juu, ujenzi wa nyumba bora pia uhamasishwe ili kuwa na mazingira mazuri zaidi yaliyoboreshwa na yenye kupendeza.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...