Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Rukia Mtingwa (kushoto) akiwaongoza baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo katika tukio la kujitolea damu lililoandaliwa na benki hiyo kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani jijini Dar es Salaam jana.
Meneja Mahusiano ya Kibiashara wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Lukemelelo Kaduma (katikati) akijitolea damu ikiwa ni sehemu ya matukio ya wafanyakazi wa NBC kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani jijini Dar es Salaam mwishoni jana. Anayemtoa ni mtaalamu wa damu kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama (NBTS), Peter Chami na kushoto ni mkazi wa Jiji la Dar es Salaam, Benard Elikana.
Mmoja wa wafanyakazi wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Jolanda Songoro (kushoto) akijitolea damu ikiwa ni sehemu ya matukio ya wafanyakazi wa NBC kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani jijini Dar es Salaam mwishoni jana. Anayemtoa ni mtaalamu wa damu kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama (NBTS), Peter Chami.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...