Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Richard Ndassa
akitoa maagizo kwa Wakandarasi, Wataalamu kutoka Shirika la Umeme Nchini
(Tanesco), Wizara ya Nishati na Madini na viongozi mbalimbali kwenye majumuisho
ya ziara ya kamati hiyo, baada ya kufanya ukaguzi wa miradi ya umeme mkoani
Singida pamoja na kuzungumza na wananchi.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Richard Ndassa
(katikati) akisisitiza jambo katika eneo la mradi wa kuzalisha umeme kwa njia ya
upepo lililopo Kisesile wilayani Singida Mjini mara kamati hiyo ilipotembelea mradi
huo ili kujionea maendeleo yake pamoja na kuzungumza na watendaji wa eneo hilo.
Na Greyson Mwase, Singida
Mkuu wa Kitengo cha Miundombinu na Nishati kutoka Shirika la Maendeleo la
Taifa (NDC) Pascal Malesa amesema kuwa serikali inatarajia kutumia Dola za
Marekani Milioni 132 kwa ajili ya kukamilisha mradi wa kuzalisha umeme wa upepo
wenye uwezo wa Megawati 50 ifikapo mapema mwaka 2016.
Malesa aliyasema hayo mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na
Madini iliyofanya ziara ya kutembelea mradi wa kuzalisha umeme kwa njia ya
upepo unaojengwa katika eneo la Kisesile nje kidogo ya Singida Mjini. Kamati
ya Bunge ya Nishati na Madini ipo mkoani Singida kwa ajili ya kukagua miradi ya
umeme ili kujionea maendeleo yake pamoja na kuzungumza na wananchi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...