Mratibu wa Mradi wa Macho kwa shule za msingi kupitia mradi wa afya ya macho kwa mtoto unaofadhiliwa na benki ya Standard Chartered (Seeing is Believing) kutoka shirika lisilo la kiserikali la Brien Holden Vision Institute Violeth Shirima (kushoto) akimkabidhi msaada wa sanduku la vifaa vya macho vyenye thamani ya shilingi milioni 48 Muuguzi Msaidizi wa Huduma za Macho wa Hospitali ya Wilaya ya Kyela, Monica Francis (kulia) wakati wa hafla iliyofanyika katika hospitali ya mkoa wa Mbeya. Wanafunzi wa shule za msingi za halmashauri za Mbozi, Ileje , Kyela watanufaika na msaada huo wa kutibiwa magonjwa ya macho bure. Wanaoshuhudia: wa pili kutoka kulia ni Kaimu Afisa Elimu wa Wilaya ya Kyela, Kassim Mtili na Mratibu wa Huduma za Macho Mashuleni, Leah Mwakakapala.
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya, Constantine Mushi akikabidhiwa msaada wa mashine ya Kompyuta inayopima macho (Autorefractor) na Mratibu wa Huduma za Macho kwa watoto wa shule za msingi kupitia mradi wa Afya ya Macho kwa Mtoto (Seeing is Believing) unaofadhiliwa na benki ya Standard Chartered, Violeth Mushi , wakati wa hafla iliyofanyika katika hospitali ya Mkoa wa Mbeya. Jumla ya vifaa vvyenye thamani ya shilingi milioni 48 vilikabidhiwa kwa hospitali za wilaya za Mbozi, Ileje na Kyela.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...