Timu ya Vijimambo ikishiriana na Kwanza Production inapenda kwanza kutoa pongezi kwa Watanzania Houston kwa jitihada zao za kupambana na mauaji ya ndugu zetu wenye ulemavu wa ngozi Pia inaandaa kipindi cha video kuongelea hili swala kwa mapana zaidi na kuangalia jinsi gani ya kukomesha mauaji haya ambayo yanaleta fedheha na aibu  ikiwemo ukiukaji wa haki za binadamu.

Kipindi kitarekodiwa siku ya Jumampili saa 8 mchana (2pm) mahali ni Extended Stay America chumba namba 224 anuani ni 2424 West Sam Houston Prkway, Houston, TX 77042. 

Wadau kutoka New York katika moja ya vipindi vilivyorekodiwa.

Wadau wa North Carolina wakiwa kwenye kipindi kilichopata kurekodiwa.

Kwa maelezo zaidi wasiana na 301 335 6383 asante

Ujumbe kutoka kwa ndugu zetu hapo chini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Mauaji yanafanyika Tanzania, kipindi kinarekodiwa Marekani, ina maana gani kama sio kuendelea kujidhalilisha ugenini?! Na itasaidia nini??

    Kinachotakiwa ni nguvu za dola zifanye kazi yake hapa nchini, hizo porojo nyingine hazina maana, NUKTA.

    ReplyDelete
  2. Ni sawa kabisa sioni shida kurekodi nje hii movie. Kama wasanii Tanzania hawashtuki kurekodi juu ya mauaji ya albino kuelimisha jamii ila wanarekodi movie za kimapenzi tu, waache walioguswa walekodi na hii aibu iendelee tu kuonesha kuwa tumeshindwa kuchukua hatua na tunahitaji majeshi ya nje yaje yatusaidie. Hakuna jinsi mimi naona ni sawa tu. Wamefanya vema

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...